Katavi.
MWANZILISHI na Mkurugenzi wa Taasisi ya NeoLife International kanda ya Magharibi,Veronica Biaka amesema dhana ya usawa wa kijisia sio kukandamiza jinsi yeyote bali ni kuweka mfumo mzuri utakaosaidia kuwa na fursa sawa kwa jinsi zote.
Dhana ya usawa wa kijinsia ndani ya jamii ya Mkoa wa Katavi imekuwa ikitafasiriwa kuwa na lengo la kumgandamiza mwanaume ambaye amekuwa kiongozi kuanzia ngazi ya familia.
Veronica ametoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa New Katavi resort Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakati akizungumza kwenye kongamano la wajasiriamali ambapo amewaondoa hofu wanaume na kuwataka kuwapa fursa wanawake ya kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi huyo wa Neolife International amesema baadhi ya watu wengi hawafahamu dhana ya usawa wa kijisia,wengine wanahusisha usawa wa kijinsia na ubaguzi au kulinda kundi moja katika jamii jambo ambalo sio kweli na linarudisha nyuma jitihada za usawa ndani ya jami
0 Comments