Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI.
Katika kuweza kujisahihisha sambamba na kwenda na dhana nzima ya ukweli na uwazi makada wa chama cha mapinduzi wametakiwa kukubali kukosolewa pindi inapoonekana kuna sehemu ambayo haupo sawa.
Kukosolewa kwenyewe kunaweza kuleta mafanikio makubwa na hasa kama mkosoaji hatakosoa Kwa mihemko ya kisiasa badala ya kuwa na dhamira ya kuleta mabadiliko chanya.
Akichangia hoja katika kundi 'zogozi'(Whatsapp)lenye kuwakutanisha viongozi na wanachama wa CCM wa wilaya ya Moshi Vijijini mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama hicho Yuvenail Shirima amewakumbusha wanachama hao kukubali kukosolewa.
"""Tunatakiwa kuwathamini na kuwaheshimu sana watu wanaosema ukweli kwetu bila kujali ukweli huo unatuuma kiasi gani."""
Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini COMRADE YUVENALI SHIRIMA
Hata hivyo baadhi ya wanachama akiwemo Marry Mariki anachangia hoja hiyo kwa kuieleza kuwa wanachama ama viongozi walio wengi hawapendi kukosolewa jambo ambalo sii rafiki katika uongozi.
'ukiwa kiongozi wewe sio malaika yaani kila kitu kiwe sawa hapana haiwezekani ni lazima tukubali kukosolewa ili kujirekebisha'anachangia
Doris Mallya anasema kuwa viongozi wengi huona kukosolewa kama ni kuvunjiwa heshima na kuwa wanaamini wanaweza kuwa sahihi Kwa kila jambo.
MWISHO.
0 Comments