Header Ads Widget

NEEMA UMEME WA REA MOSHI VIJIJINI RASMI.....

 Na Gift Mongi

MATUKIO DAIMA APP MOSHI.

Wakazi wa maeneo ya Arusha Chini na Mabogini katika jimbo la Moshi Vijijini wapo mbioni kupata huduma ya umeme wa uhakika kutokana na maandalizi yake kuanza na wakandarasi tayari wapo kazini tayari kwa utekelezaji mradi huo.

Taarifa kutoka katika ofisi ya mbunge wa jimbo hilo kwa sasa Prof Patrick Ndakidemi zinaeleza kuwa tayari wakandarasi wameanza kutekeleza mradi huo mapema mwezi huu.

Taarifa hiyo kwenda kwa vyombo mbali mbali vya habari vya habari inaeleza kuwa kampuni ya OK Electrical Service LTD itapelekea umeme katika kata ya Arusha Chini Vijiji na maeneo ya Mikocheni Ndogo  Chemchem  na Chemchem Shuleni      


'Mkandarasi huyu tayari yupo kazini kwa ajili ya kusambaza nguzo kwenye maeneo husika lengo likiwa ni kutekeleza ahadi Kwa wananchi'inaeleza

Aidha kampuni ya DIEYNEM COMPANY LIMITED atatekeleza pia  mradi katika kata ya Mabogini katika Vijiji  na maeneo ya Mtakuja TRF 1,Shabaha, Mtakuja TRF 2
na  Upareni

Ata hivyo taarifa inafafanua kuwa mkandarasi huyu ameshafika kuyaona maeneo ya mradi na anajipanga kuanza kazi hiyo. Tayari amejitambulisha katika Kata na Vijiji husika.

Mkazi wa Mabogini Isaya Mwita anasema kupatikana kwa umeme katika eneo lao kunaenda kukuza shughuli nyingi za uzalishaji na kujiingizia kipato.

'Ukishakuwa na umeme shughuli nyingi zitaweza kufanyika lakini pia Kwa vijana wanaweza kujiajiri katika sekta mbalimbali'amesema
MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI