Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP DODOMA
TAASISI ya uthibiti ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imesema imeweza kudhibiti tatizo la uzalishaji Mbegu feki hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha kuwa na mazao yenye tija ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani watu ambao walijihusisha na uzalishaji wa Mbegu feki.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo,PATRICK NGWEDIAGI ameyaeleza hayo Jijini Dodoma wakati akitoa Taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya TOSCI na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
" Kama taasisi tumeweza kudhibiti tatizo la uzalishaji mbegu feki hapa nchini na lengo letu lilikuwa kumpatia mkulima mbegu bora na kuleta tija kwenye mazao," Amesema NGWEDIAGI.
Pamoja na hayo,NGWEDIAGI amebainisha kuwa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Taasisi ya TOSCI,inatarajia kutumia jumla ya Shilingi Bilioni12.6kwaajili ya kutekeleza Mradi wa Sekta ya Kilimo na Uvuvi ikiwemo Kujenga Maabara kubwa ya kisasa ambayo itaweza kuchambua na kupima ubora wa Mbegu.
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kutokana na Mbegu zinazozalishwa kuzingatia ubora, jumla ya Tani elfu nne,zimeuzwa nje ya Nchi.
Taasisi ya uthibiti ubora wa Mbegu Tanzania hivi sasa imeweza kuongeza ufanisi wa uzalishaji Mbegu zenye ubora kwa asilimia 75 Toka asilimia 35 ambapo ni ongezeko kubwa.






0 Comments