Header Ads Widget

TFS YAZALISHA TANI 25 .9 ZA MBEGU ZA MITI

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


KAMISHNA wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS ) Prof. Dos Santos Silayo amesema, Kwa mwaka wa fedha uliopita, TFS ilizalisha jumla ya tani 25.9 za mbegu za miti na kuotesha miche 32,735,653 ya aina mbalimbali.


Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Kamishna huyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na na kuekeza kazi zinazofanywa na Wakala wa Misitu Tanzania.


Miti hiyo ilipandwa katika mashamba 24 ya Serikali na mingine kugawiwa kwa watu binafsi, taasisi na mashirika mbalimbali kwa ajili ya kupandwa katika maeneo yao. 


"Hadi sasa, TFS imepanda miti katika hekta 6,909 na kurudishia miti iliyokufa kwenye hekta 2,434," Amesema Prof Silayo. 


Vilevile Amesema, Wakala umeendeleza mashamba ya miti kwa kupalilia hekta 31,197, kupogolea hekta 8,353 na kupunguzia miti kwenye hekta 2,785. 


Katika hatua nyingine, Wakala umeandaa Mkakati wa Usimamizi na Uendelezaji wa Mashamba ya Miti ya Serikali wa Miaka 30 (2021 - 2050) ambao umelenga kupanua wigo wa aina ya miti ya ikiwemo ile ya madawa kama vile Prunus africana na mpira (rubber). 


"Miti hii imeanza kupandwa katika mashamba ya Mbizi, Wino, Rongai, Saohill, Iyondo Mswima, Meru na Shume," amesema Prof Silayo.


KUENDELEZA UTALII IKOLOJIA NA UTAMADUNI


Amesema Kufuatia juhudi za makusudi zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo ubunifu wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuandaa filamu ya “Tanzania the Royal Tour” ambayo imetangaza nchi yetu ndani na nje ya nchi kwa kiasi kikubwa, TFS imejipanga kutumia fursa hiyo kuongeza tija katika uhifadhi, utalii na ukusanyaji maduhuli. 


Amesema Juhudi zilizofanyika zimewezesha kuongezeka kwa idadi ya watalii waliotembelea vivutio vya utalii ikolojia ambapo hadi kufikia Juni 2023 jumla ya watalii 242,824 walitembelea vivutio hivyo. 


"Idadi hii ni ongezeko la asilimia 60.8 ukilinganisha na watalii 152,002 waliotembelea vivutio hivyo kwa kipindi hicho kwa mwaka 2021," Amesema .


Na kuonge"Jumla ya Shilingi 1,368,940,965 zilikusanywa ikilinganishwa na Shilingi 603,311,740 zilizokusanywa mwaka uliopita ikiwa ni ongezeko la Asilimia 126.9.  Takwimu hizi zinaweka rekodi mpya kwani Wakala haukuwahi kufikia malengo haya hapo kabla," Amesema Prof Silayo. 


Hata hivyo Amesema Katika kipindi cha mwaka jana pia TFS ilipewa fedha kiasi cha TZS 4 Bilioni kutoka sehemu ya fedha alizotoa mheshimiwa rais kuboresha uhifadhi na shughuli za utalii katika misitu yetu. 


"Tumekamilisha kwa ufanisi ujenzi wa malango 5 katika hifadhi 5, Ujenzi wa barabara urefu km 97 na njia za kutembea kwa miguu km 190.5 katika hifadhi 11," Amesema


Aidha, kupitia mpango kazi wa ndani wa taasisi TFS imeendeleza vivutio vya utalii wa kiikolojia na kiutamaduni kwa kukarabati kilomita 231.7 za njia za watalii na kilomita 643.54 za barabara za msituni; na kuandaa ramani za vivutio vya kiikolojia katika misitu ya hifadhi. 


Amesema Wakala umekamilisha ujenzi wa hosteli 2 moja katika msitu wa Wino, Songea na nyingine katika msitu wa SaoHill, Mafinga Iringa na kukarabati hosteli moja katika hifadhi ya Mazingira Asilia Amani.


Ameeleza , makambi sita (6) ya watalii katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Kilombero, Magamba na Mlima Hanang yamekamilishwa ambapo ujenzi wa banda 1 la kupumzika watalii, mageti matatu (3) na mabango 8 katika vituo vya Michoro ya Miambani Kolo – Kondoa na Magofu ya Tongoni – Tanga. 


Pia, utengenezaji wa benchi 8, meza 3 umefanyika katika Shamba la Miti West Kilimanjaro na pia miundombinu mingine mingi kuwezesha utalii katika misitu mbalimbali.


Amesema Wakala umeendelea kutangaza vivutio vya utalii ikolojia, utamaduni pamoja na uhifadhi wa rasilimali za misitu kupitia maonesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ikiwemo Sabasaba, Nanenane, Tanga Trade Fair, International Tourism Expo Japan 2022, East Africa International Tourism Expo, S!TE na 2022 World Cup. 


Amebainisha wakala kwa kushirikiana na wadau uliandaa mashindano ya utalii maarufu kama West Kili Forest Tour Challenge, Bata Msituni Festival, na Sao Hill Forest Rally. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI