Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Jumuiya na Taasisi za kiislamu Tanzania imeishukuru Serikali kupitia Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Taasisis ya elim Tanzania TET kwa kukubali kuacha suala la mitaala ya dini libaki kwa wenye dini wenyewe huku ikikubali kuboresha katika mambo ya kitaalam.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya jumuiya hiyo kukutana na waandishi wa habari ikiomba kukutana na Waziri Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda mara baada ya kupata taarifa kuwa serikali inataka kuchukua mitaala ya dini .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Amir Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Alhaj Sheikh Mussa Kundecha, amesema kuwa wanaipongeza na kuishukuru Serikali mara baada ya kuridhia kukutana nao kukubaliana katika jambo hilo.
Amesema kuwa, suala la dini na imani haliwezi kutenganishwa kwani imani ndio msingi wa mafundisho ya dini, hivyo wamemshukuru waziri kwa kutoa ushirikiano mkubwa na hatimae kuliweka sawa jambo hilo, hivyo wnamshukuru sana Waziri kwa kutoa ushirukiano mkubwa.
"Ndugu wanahabari tarehe 10 mwezi huu, tulikutana nanyi kueleza suala la Serikali kumiliki mtaala wa somo la dini ya kiislam lakini pia katika somo hilo mambo yote ya imani yanayohusiana na dini yataondolewa, baadae tukaomba kukutana na waziri mwenye dhamana, akatusikia ombi letu na kukubaliana nae tunamshukuru sana"amesema Sheikh Kundecha.
Aidha, amesema kuwa walikutana na na Waziri wa elimu siku ya jumamosi akiwa na waatalamu wake wa taasisi ya elimu Tanzania, ambapo walizungumza jambo hilo na kukubaliana kwamba somo la dini libaki kwa wenye dini wenyewe






0 Comments