Header Ads Widget

TAKUKURU PWANI YABAINI SOKO KUTOTOA RISITI ZA EFD

 


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Pwani imebaini wakusanyaji wa ushuru kwenye soko la Mnarani Halmashauri ya Mji Kibaha kutotoa risiti za mashine (EFD) baada ya wafanyabiashara kufanya malipo kwa kisingizio cha ubovu wa mashine hizo.


Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Takukuru mkoani humo Christopher Myava alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.


Alisema kuwa sababu nyingine ya kutotoa risiti hizo wanasema kuwa eti mashine hazina chaji hali ambayo inasababisha wakusanyaji kutumia fedha hizo kwa matumizi yao binafsi.


Aidha alisema kuwa kutokana na hali hiyo kunakosekana kumbukumbu za wafanyabiashara waliofanya malipo hivyo kusababisha upotevu wa mapato.


Alisema kuwa mradi mwingine ambao ulibainika kuwa na changamoto ni mzabuni aliyechaguliwa kupeleka vifaa vya ujenzi shule ya sekondari ya kata ya Shungubweni Halmashauri ya Mkuranga kutoomba kazi hiyo kwenye mfumo wa serikali wa TANEPS.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI