Header Ads Widget

KUNENGE ATAKA HALMASHAURI ZIONGEZE MAPATO

 



MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezitaka Halmashauri Mkoani humo kushirikiana Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupata ya namna ya kuongeza ukusanyaji wa mapato. 


Kunenge aliyasema hayo Mlandizi wakati akizungumza na wataalamu mbalimbali na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa akifungua mafunzo ya namna ya kuongeza mapato kwenye Halmashauri kupitia mpango wa miaka mitano wa (Mpango Mkakati wa Kuongeza Mapato) yaliyoandaliwa GIZ.


Alisema kuwa Halmashauri kupata mafunzo hayo kutasaidia lengo la kuongeza mapato pia watumie teknolojia ili kukusanya mapato ambapo mapato yakiongezeka itasaidia kuipa uwezo serikali kuhudumia wananchi wake.


Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa George Nsajigwa Mpango Mkakati huo wa Kuongeza Mapato kwa Halmashauri hapa nchini uko kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Pwani ambapo ndo mkoa wa kwanza kufanya mafunzo hayo.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana ambapo malengo yao kwa Halmashauri ya Kibaha Mji ni kufikia makusanyo ya shilingi bilioni 30 na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kukusanya bilioni 20 katika kipindi cha miaka mitano.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kupata mbinu mpya za ukusanyaji wa mapato ambapo kwa mwaka jana Halmashauri hiyo iliongoza kwa ukusanyaji mapato.


Mwezeshaji wa mafunzo hayo Peter Laizer mshauri wa mradi wa utawala bora wa fedha kutoka shirika hilo alisema kuwa mafunzo hayo yatawahusisha wataalamu wa masuala ya fedha kwenye Halmashauri kushirikiana na vitengo vingine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI