Na,Jusline Marco,Matukio Daima App Arusha
Halmashauri ya Arusha imetoa vyeti vya pongezi kwa shule za sekondari zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita zilizoshika nafasi ya kumi bora kiwilaya na kimkoa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha Seleman Msumi akizungumza wakati wa utoaji wa vyeti hivyo vya pongezi kwenye kikao cha baraza la madiwani, amesema kuwa takribani shule 5 zimeweza kuingia kwenye 10 bora ya mkoa ambapo katika matokeo ya kidato cha 6 halmashauri hiyo imeweza kuwa ya kwanza kimkoa.
Aidha amesema katika kutambua mchango wa walimu wao na wanafunzi waliojituma kuweza kuiheshimisha halmashauri na mkoa kwa ujumla, halmashauri hiyo imeona kuweka utaratibu wa kutoa vyeti hivyo vya pongezi kwa kata husika na katika shule zilizofanya vizuri.
Pamoja na hayo Msumi ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa fedha walizozitoa katika halmashauri hiyo kiasi cha shilingi bilioni 2 kupitia programu ya Uviko na kuganikiwa kujenga madara 100 ikiwemo madara 4 ya shule shikizi na madarasa 96 kwa ajili ya shule za sekondari.
Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa baraza la madiwani ,Ojung'u Sarekwa amewataka madiwani wa baraza hilo kutumia kikao hicho kama sehemu ya kufanya mrejesho wa yale yaliyofanywa na halmashauri hiyo kwa muda wa mwaka mzima.
Katika mwaka wa fedha ulioisha halmashauri hiyo iliweza kupata fedha shilingi bilioni 720 na kufanikiwa kujenga madarasa 32 kwenye shule 18 za sekondari huku katika mradi wa boost halmashauri hiyo ikipokea fedha za elimu msingi na sekondari kiasi cha shilingi bilioni 14.
0 Comments