NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amewataka wakaguzi wasaidizi wa jeshi la polisi walioko Kila kata kufanya kazi Kwa weledi pasipo kumuonea mtu na kufata misingi ya sheria.
Haya ameyasema wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya polisi jamii yaliyofanyika Jijini hapa yakiwa na lengo la kuongeza ushirikiano baina ya wananchi na jeshi la polisi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Makalla Amesema kuwa Kwa kushirikiana na watendaji na wenyeviti wa mitaa na vijiji kutaweza kumailisha Usalama na amani kuimalika pamoja na Maendeleo kupatikana kwenye sekta mbalimbali.
"Hivi sasa Kila mmoja ni mwandishi wa habari , na anatoa taarifa hiyo yote ni Kwa sababu Dunia ya sasa iko kidigitali zaidi, Kila mtu anatoa taarifa wakati mwingine hali inakuwa shwali lakini mtu mwingine anaamua kuchukua video za zamani na kusambaza na kusema tukio hilo limetokea Jana na kuendelea kuwapa hofu watu." Alisema Makalla
Kamishina wa kamisheni ya polisi jamii Faustine Shilogile ameeleza kuwa watendaji waendelee kutoa ushirikiano lengo ni kuhakikisha ushirikiana unakuwepo Kwa wananchi na wanaendelea kuwa salama.
"Tuliamua kuanzisha zana hii ya jamii polisi Kwa kuwa polisi tuko wachache hatuwezi kuingia Kila sehemu ya Nchi yetu ndio lengo letu la kuanzisha jamii polisi" Alisema Faustine.
Faustine ameeleza kuwa hakuna mradi wowote unaweza kuanzishwa ukawa hauko kwenye eneo la kata ili kuendelea kulindwa na kuwa salama.
"Kama uko kwenye kata inamaana Kuna askari kata anaulinda, linapotokea lolote lile lla kutokea ni lazima tumuulize askari kata na mtendaji wa eneo hilo imekuwake tukio hilo likatokea" Alisema Faustine.
Kwa upande wake Kamishina msaidizi wa Jeshi la polisi Mstaafu Engelbert Kiondo amesema kuwa jeshi hilo tangu mwaka 60 baada ya uhuru limekuwa likifata taratibu za wazungu Kwa muda mrefu kazi ulifanyika mpaka miaka ya 2000 upolisi ulifanyika Kwa maagizo na sheria tu bila kujali masilahi ya wananchi.
" Polisi inajukumu la kufanya jamii iwe salama na kuwa na Maendeleo endelevu, na sio kazi ya kupiga virungu kutishia watu na kuwapiga mabomu"Kiondo.
0 Comments