Header Ads Widget

PSSSF YAWALIPA WANUFAIKA TRILIONI 88.8

 


Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeongeza thamani ya mfuko huo kwa kupitia uwekezaji na kufanikiwa kuwalipa wanufaika 262,09 Jumla ya shilingi Trilioni 8.88, katika kutekeleza majukumu yake.



Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba amesema kwa kipindi cha miaka mitano Mfuko wa PSSSF umetatua changamoto nyingi na kupata mafanikio makubwa kwa kulipa madeni ya kiasi cha shilingi Trilioni 1.03, yaliyorithiwa kutoka kwenye mifuko iliyounganishwa kwa wanufaika 10,273.


Mkurugenzi amesema kuwa madai haya yalilipwa ndani ya miaka miwili, huku mfuko ukiendelea kulipa madai mapya ya kiasi cha jumla ya Trilioni 8.88, kwa wanufaika 262,095, ambayo imeongeza thamani ya uwekezaji kwa 23.5% kutoka Trilioni 6.40, hadi Trilioni 7.92, ambalo ni wastani wa ongezeko wa asilimia 4 kwa mwaka, kupata mapato yatokanayo na Uwekezaji wa wastani wa asilimia 85 kwa mwaka, kumeongeza thamani ya mfuko kwa 27.76% kutoka Trilioni 5.83 hadi Trilioni 8.07, sawa na wastani wa ongezeko la 6.12% kwa mwaka.




"Kupunguza gharama za uendeshaji kutoka wastani wa 12% hadi 5% ya mchango inayokusanywa kwa mwaka ikiwa ni chini ya ukomo wa 10%, kwa mujibu wa taratibu za kanuni, kulipa bila kukosa na kwa wakati pensheni ya kila mwezi, wastani wa shilingi Billioni 67 kwa wataafu kila ifikapo tarehe 25 ya mwezi husika" amesema Hosea.


Amefafanua kuwa hii ni ongezeko la asilimia 100%, ukilinganisha na kiasi cha wastani wa shilingi Billioni 34 wakati wa kuunganishwa, pia Mkurugenzi ameongeza kuwa wamefanikiwa kupunguza muda wa kusubili mafao, kwani mfuko unalipa ndani ya siku 60, kwa mujibu wa sheria, na kabla ya mfuko Wastaafu wengine walitumia zaidi ya miaka mitatu kusubili mafao yao.



"Kuboreshwa huduma za wateja kwa kutumia mifumo ya TEHAMA iliyovumbuliwa, kutengenezwa na kuendeshwa na wataalamu wetu wa ndani kwa 90%, uwaunganisha Wafanyakazi wote waliotoka kwenye mifuko mingine iliyokuwa na tamaduni tofauti na sasa wana lengo moja la kazi za mfuko mpya" amesema CPA Kashima.


Hata hivyo Kashima amefafanua kuwa PSSSF inatenda kazi kulingana na sheria, taratibu na mwongozo wa Serikali ukaguzi wa wa Mahesabu na Manunuzi, mfuko umepata hati safi za hesabu za mfuko toka uanzishwe na pia umepata tuzo za uandaaji na uwasilishaji bora wa mahesabu kutoka NBAA, kwa miaka miwili mfululizo (2020/2021 -2021/2022.



"Tunatekeleza kikamilifu taratibu za manunuzi ya Umma, mwaka 2020/2021, mfuko ulishika namba kwa Taasisi za Serikali kwa kupata matokeo ya 94% ya ukaguzi wa uzingatiaji wa miongozo ya manunuzi ya Umma" amesema CPA Hosea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI