Header Ads Widget

NYUMBA YA MBAO YENYE ZAIDI YA MIAKA 100 YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO HAWAII, MAREKANI.


Na Matukio Daima App, Hawaii, Marekani.

Picha zimesambaa sana za nyumba moja yenye paa jekundu ambayo inaonekana haijadhurika kwani mtaa unaoizunguka umepunguzwa na kuwa marundo ya majivu na vifusi kutoka kwa moto wa Maui.


Nyumba ya mbao yenye umri wa miaka 100 kwenye Mtaa wa Mbele bado imesimama kwani sehemu kubwa ya mji wa Lahaina imeharibiwa.


"Inaonekana kama picha ya kutengenezwa (photoshop)."

Picha za nyumba hii iliyonusurika kuteketea kwa moto huko Maui zimesambaa mitandaoni.

Nyumba hiyo iliyoezekwa kwa paa jekundu huko Lahaina bado imesimama huku mtaa wote unaoizunguka ukiwa umeteketea na kusalia vifusi na majivu jivu.

Wamiliki wa nyumba hii wanasema wanahisi "wana hatia" kwamba nyumba yao, ambayo imejengwa kwa mbao na ina umri wa angalau miaka 100, ilinusurika wakati nyumba jirani zimeteketea.

"Ni nyumba ya mbao 100%, wala hatukutumia mbinu yeyote kuzuia moto " Dora Atwater Millikin aliambia Los Angeles Times.

Bw Millikin na mkewe walisema hawana uhakika ni nini hasa kiliokoa nyumba hiyo walioinunua kutoka kwa mtunza hesabu wa wafanyakazi wa shamba la sukari enzi za ukoloni.


Bw Millikin na mkewe walikuwa safarini mkasa huo wa moto ulipozuka na wanasema kuwa nyumba hiyo ilikuwa mbovu, hivyo walitaka kuirejesha katika ubora wake.

Huenda ukarabati huo ndio uliookoa nyumba hiyo.

Walibadilisha paa la lami la nyumba na kuweka mabati yenye-kipimo kizito, wakajenga ya kwa mawe na kuondoa miti maua na majani yaliyokuwa yameizunguka.

Lakini hakuna hata moja ya vitendo hivi vilivyokusudiwa kuzima moto, walisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI