Header Ads Widget

NMB YAKABIDHI T-SHETI KWA BENDI YA JKT


Na Hadija Omary-Matukio Daima App, Lindi.

 

Benki ya NMB Kanda ya kusini imesema itaendelea kuunga mkono jitiada za Serikali katika  kuhakikisha Sekta ya michezo inaendelea kuimarika hapa Nchini

 

Hayo yamebainishwa na Afisa mauzo wa Benk ya (NMB) kanda ya kusini Romani Degeleki jana wakati wa ghafla ya makabidhiano ya T-SHERT  kwa ajili ya Bendi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT) iliyopo Wilayani Nachingwea yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lindi Mkoani Lindi

 

Degeleki  amesema Benk hiyo  imekuwa na utamaduni wa kutoa vifaa mbali mbali vya michezo  ili kuinua sekta hiyo hapa Nchini ikiwa ni moja ya kurudisha faida waliyoipata kutoka kwa wateja wao

 

“Kwa bendi hii ya JKT tumejiwekea pia utaratibu kupitia maonyesho haya ya nanenane lazima tuivalishe na tuipendezeshe Bendi hii ili iweze kutoa burudani mzuri kwa wakazi wa Lindi na wa mikoa jirani ambao  kwenye nane nane hii”

 

 

Kwa upande wake Luteni Kanali Nyangalu Malecela Kamanda kikosi cha (JKT) Nachingwea pamoja na kuishukuru Bank hiyo kwa kutambua mchango wa Jeshi la kujenga Taifa katika nyanja ya Michezo pia alisema kuwa kitendo cha NMB kurejesha wanachokipata kwa jamii inayowazunguka kitawafanya wateja wao kuendelea kuwa na imani na huduma wanazozitoa.

 

“Tunawashukuru sana NMB kwa sababu sare hizi ambazo mmetupatia leo zitaenda kuboresha kikosi chetu cha bendi lakini pia itakuwa kama motisha kwao kuweza kufanya vizuri zaidi ”alieleza  Luteni kanali Malecela


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI