Header Ads Widget

NJOMBE SAIDIENI YATIMA

                   

"Watoto yatima wanahitaji msaada na faraja "                               



 Na Frederick Siwale - Matukio Daima App ,Makambako.           


WANANCHI mkoa wa Njombe wameombwa kusaidia Watoto yatima wanaolelewa vituoni ili kuwapa faraja maishani mwao.                                


Rai hiyo imetolewa na mtawa Sir.Tumaini Ndumbalo  wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Tumaini Ilunda kilichopo parokia ya Mtwango Halmashauri ya wilaya ya Njombe.                       


Mtawa Sir.Ndumbalo alisema hayo wakati akipokea msaada wa vitu mbali mbali kutoka kwa Umoja wa Machinga stendi mpya ya mabasi Makambako wakishirikiana na Taasisi ya umoja wa amani kwanza ( UAK) mkoa wa Njombe.             


Alisema anawashukuru wadau hao pamoja na Wadau wengine walioshiriki kupata vitu hivyo vikiwepo vyakula ,mafuta ya kupikia na kupakaa , Sukari, Mchele ,viazi mviringo ,sabuni na nguo.   


Sir.Ndumbalo alisema kituo hicho kina jumla ya Watoto 52 wanaolelewa kituoni hapo huku 14 wakiwa wanasoma shule za msingi na Sekondari.       



"Kituo Watoto kituoni wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja ukosefu wa bima za afya kwani ikitokea Watoto 10 wameugua basi changamoto inakuwa gharama za matibabu"                          


Pamoja na kuwashukuru wadau waliofika kituoni hapo alitoa wito kwa Wananchi katika Halmashauri za Wilaya ya Njombe, Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri ya mji Makambako kuona haja ya kuwatembelea   kituoni Watoto hao Yatima na kutoa misaada kibinadamu.

 

" Wasaidieni Watoto katika vituo vya Yatima ili na wao wajione kuwa Wana Wazazi badala ya kuonekana ni Yatima waliotengwa na Jamii kwa uyatima wao ambao hawakujipendea"                    


Akisisitiza Sir.Ndumbalo aliomba jamii kuiga mfano wa Wamachinga kwa kushirikiana na Taasisi ya Umoja wa amani kwanza (UAK) katika moyo wa huruma na upendo kwa wenye uhitaji.             



Alisema inafahamika kuwa katika mkoa wa Njombe zipo taasisi nyingi na Wafanyabiashara wakubwa wenye uwezo wa kusaidia na wengine ambao wakishirikiana Yatima hawa wanaweza kujikuta sawa na Watoto wengine wenye Wazazi wao.       


Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wamachinga stendi ya mabasi Makambako Bw.Abasi Mdemu, alisema ujio wao ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Chinga day ambayo wao walichinja ng'ombe na kula na kunywa na hivyo wakaona iko haja ya kugeukia kwa wahitaji ambao ni Watoto Yatima .                             



Bw.Mdemu alisema wazo hilo liliungwa mkono na Wadau mbali mbali ikiwepo Taasisi ya Umoja wa amani Kwanza Tanzania mkoa wa Njombe ili kutimiza adhima na kiu yao ya kushiriki kugawa upendo, amani na faraja kwa wenye uhitaji.


Aidha upande wao Bi.Jonisia Sanga , Bw.Salumu Hassan na  Bi.Otavina Longole walisema wamefarijika sana kufika kuwaona Watoto hao Yatima na kuwabeba katika kuonyesha mapenzi mema na upendo wa agape na kwamba kurudi ni lazima watarudi kuwatembelea tena Watoto hao na kwamba pongezi na shukrani za pekee ni kwa Masista na Walezi wa Watoto hao kwa kazi kubwa wanayoifanya.                      



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI