Header Ads Widget

NJOMBE DC KUHESABU UBAO KWA UBAO ILI KUDHIBITI UTOROSHWAJI MAPATO

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP Njombe 


Halmashauri ya wilaya ya Njombe imeshindwa kufikia asilimia 100 katika ukusanyaji mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha  wa 2022/2023 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kushushwa  kwa ushuru wa mbao.


Asilimia 98 za ukusanyaji mapato ndizo zilizofikiwa na sababu kubwa ni kufanyika kwa marekebisho ya tozo za mbao kutoka Shilingi 200 Hadi shillingi 100 kwa ubao kwa maelekezo ya serikali kuu.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli wakati akifungua mkutano wa Kawaida wa baraza la madiwani amesema pamoja na Changamoto hiyo lakini uzembe wa baadhi ya maofisa watendaji katika kukusanya maduhuri hayo ya serikali ni miongoni mwa kikwazo cha kukwamisha malengo hayo.


Hongoli Amesema serikali ilitoa pikipiki kwa maofisa watendaji wa kata hivyo hataki kusikia sababu yoyote ya kutofuatiliwa kwa makusanyo kwenye vijiji.


Baadhi ya madiwani akiwemo Vasco Mgunda na Neema Mbanga wamesema uzembe unaofanywa na baadhi ya maofisa watendaji katika ukusanyaji mapato unasababisha wafanyabiashara Wengi kutoroka na fedha jambo ambalo linapaswa kudhibitiwa.


Kwa Upande wao baadhi ya maofisa watendaji wa kata akiwemo Nyagenge Bwire,Jimson Mwanza na Maria Mbwambo  wameeleza mikakati ya kwenda kukusanya mapato hayo ikiwemo kwenda  kuhesabu ubao kwa ubao kwenye magari kauli iliyoungwa mkono na baraza Hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI