MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametangaza vita mpya na wafugaji wavamizi ambao wamekuwa wakisababisha mauaji, ubakaji na uharibifu Kwa wananchi wa wilaya hiyo kuwa hawatakuwa na nafasi tena ya kufanya matendo hayo.
Kauli hiyo ametoa baada kuona wafugaji wameeendelea kufanya matukio mbalimbali katika wilaya hiyo bila hata woga wowote ule.
Moyo alisema kuwa ameingia vitani hivyo hawezi kurudi nyuma katika vita atasonga mbele hadi ashinde vita hiyo ambayo imedumu Kwa miaka mingi wilaya ya Nachingwea.
Awali wananchi na madiwani walimueleza mkuu wa wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo namna gani ambavyo wafugaji wamekuwa wakileta madhara kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila aliwataka viongozi na wananchi kuacha tabia ya kuuza ardhi kihorela bila kufuata taratibu za sheria na kanuni za nchi Kwa kufanya hivyo ndio kunasababisa wafugaji kuvamia maeneo ambayo hayapangwa Kwa ajili ya mifugo.
0 Comments