Na Johnson Jumanne, Matukio Daima App.
Ni tayari Vital'O wanakubali bao la pili mbele ya Simba kwenye uwanja wa Estadio Benjamin Mkapa bao lile linafungwa na John Bocco baada ya kazi nzuri ya Bernard Morrison unaikumbuka mtu wangu.
Ni kwenye tamasha kubwa la mpira la Simba, Wanaita Simba Day. Ni Simba ya 2020. Vital'o wakiwa wageni wanakufa goli 6 bila majibu kifupi hawakuwa na timu ya kuifunga Simba.
Katikati ya Dimba la Simba kuna miguu ya kijana mmoja fundi hivi, Kijana yule alikuwa akitumia mguu ambao wanatumia wakina Riyard Mahrez, Mesut Ozil, Alikuwa Magician katikati ya kiungo cha Simba.
Mgongoni mwake alivaa jezi namba 8 Ni nani alikuwa? Alikuwa Rally Bwalya kijana mmoja kutokea kwenye ardhi ya Mzee Kenneth David Kaunda kule Zambia.
Jioni ile alitufunza namna ya kucheza Central Midfielder, Alitokea katikati na sura ya Xavi Hernandez anaetumia mguu wa kushoto kuna nyakati alishuka kama Deep lying playmaker kama Andrea Pirlo, Nani hakufurahi siku ile.
Pasi zake zilikuwa tamu na za kubembeleza, Alitupa za karibu kwa Jonas Mkude aliyecheza chini yake akampa tamu Said Ndemla aliecheza mbele yake na alitupa mbali kwa washambuliaji wa pembeni(Dilunga+Morrison) rejea bao la kwanza na la pili.
Alikuwa maana halisi ya kiungo wa kati, Simba walikuwa na mtu sahihi, Alikuwa Magician,Maestro,leftfooter wa VPL wakati ule alikuwa soft touch wa ukweli kabisa.
Baadaye Ndoa ya Rally Bwalya na Simba ikafikia mwisho, Ndivyo ilivyo huwa wanakuja na kuondoka ndio maisha ambayo wanaishi.
Miguu yake iliibariki ligi yetu tukaziona sana soft touch zake lazima tuwe mashahidi wa hilo ubora wake haukuwa wa kubahatisha unakumbuka tukio gani tamu kutoka kwa Rally Bwalya.
Unakumbuka ile Perfomance yake dhidi ya FC Platinum? Ni siku ile anawatawanya watoto Robert Mugabe kutoka pale Zimbabwe katikati ya kiungo. Vipi kuhusu ile assist yake kwa Captain John Bocco.
Vipi zile danadana katikati ya Fathi na Tawfiki ile mechi dhidi ya Al Ahly au siku ile As Vita anakufa miguu ya meza na vipi ule ufundi wake kwenye Simba Super Cup dhidi ya Al Hilal na Tp Mazembe, Aliwahi kupita mtoto wa Kenneth Kaunda Magician Rally Bwalya








0 Comments