Header Ads Widget

MOI KUTENGENEZA MIKONO YA UMEME.

Na Hamida Ramadhan-Matukio Daima APP, Dodoma.


MKURUNGEZI Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo (MOI ) Prof Abel Makubi Amesema taasisi hiyo imeanzisha huduma mpya ya utengenezaji wa mkono wa umeme ambapo tayari wagonjwa 5 wameshahudumiwa gharama zake ndani ya nchi ni Tsh milioni 15 na nje ya nchi ni milioni 30 mpaka 60.


Hayo yameelezwa leo Jijini hapa na Mkurungezi huyo Wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji wa majukumu hiyo


Pia Amesema Serikali imekuwa ikiwahudumia Wananchi Wasiokuwa na Uwezo kupitia MOI ilitoa misahama yenye gharama ya TZS 6.5 billioni kwa miaka miwili kwa Wananchi wasio na uwezo na ambao pia hawakuwa na Bima za afya ili kuwawezesha kupata Huduma za Uchunguzi, madawa na upasuaji.


"Kuzijengea uwezo Hospitali za Kanda/Mikoa Taasisi ya MOI kusogeza huduma kwa Wananchi wa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Tabora, Zanzibar, Kilimanjaro, Mwanza, Dodoma, Mbeya ambapo jumla ya wagonjwa 5,207 walihudumiwa katika kliniki za kawaida na wagonjwa 1,701 walifanyiwa upasuaji.Huduma ya kliniki jongefu (MOI MOBILE CLINIC) zaidi ya wagonjwa 898 wameshahudumiwa katika Wilaya ya Temeke, Bagamoyo, Kigamboni na Ilala," Amesema.


Aidha, huduma za Telemedicine zimefungwa MOI kwa ajili ya kusaidia kutoa ushauri wa uchunguzi na Tiba kwa Hospitali za Kanda na mikoaTaasisi imeendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa hospitali kubwa za Bugando, Mbeya, KCMC, Benjamin Mkapa, Hospitali ya rufaa ya Nkinga-Tabora na Mnazi mmoja Zanzibar ili waweze kutoa baadhi ya huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa MOI.


Katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar zaidi ya wagonjwa 30 wamefanyiwa upasuaji wa kubadilishiwa Nyonga na magoti na Madaktari Bingwa wa MOI ambapo zaidi ya wagonjwa 100 walihudumiwa katika kliniki za wagonjwa wa nje. 


Ushirikiano na Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifaKatika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita, Taasisi ya MOI imeanzisha na kuendeleza ushirikiano mzuri na Taasisi za kimataifa za nje katika kufanya kambi za upasuaji wa wagonjwa, mafunzo kwa wataalamu wetu, Tafiti na misaada ya vifaa Tiba ..

Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Greson Msigwa amewataka Wananchi kujenga utamaduni wa kwenda kupata matibabu hospitalini, Serikali yetu imefanya mapinduzi makubwa katika kuimarisha huduma kwenye hospitali yetu ya MOI na zingine nchini, wananchi zitumieni, msikae na wagonjwa nyumbani na msiwapeleke wagonjwa tiba mbadala (waganga wa kienyeji), msisubiri wagonjwa wazidiwe na kuwapeleka wagonjwa hospitali wakiwa wameshafika katika hali mbaya.


Amesema Serikali imejenga, inajenga na inaendelea kuboresha huduma za matibabu katika hospitali zote kuanzia ngazi ya Wilaya katika kutoa huduma za kibingwa na kibobezi, vile vile Serikali imeanza kujenga vituo vya afya kuanzia ngazi ya Kata.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI