Kukamilika kwa Mfumo wa Makasha yanayotumia Umeme kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa ambazo zinaweza kuharibika kutokana na Joto kutawezesha Wakulima mbalimbali wanaotaka kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya Nchi kupitia bandari ya Tanga, Kusafirisha bidhaa hizo bila kuharibika.
Hayo yamesemwa na Afisa Masoko na Huduma kwa Wateja wa bandari ya Tanga Bi Habiba Godigodi wakati wa Maonyesho ya Wakulima Nanenane kanda ya Mashariki Mjini Morogoro.
Bi Habiba amesema kuwa kulikuwa na changamoto kwa Wakulima wanaosafirisha bidhaa kama Matunda mbalimbali pamoja na Maua kushindwa kusafirisha bidhaa hizo kutokana na kutokuwepo kwa njia sahihi ya kuhifadhi bidhaa hizo hivyo bandari ya Tanga imetengeneza eneo maalum la kuhifadhia makasha yenye mfumo wa umeme ili waweza kuhifadhi wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa hizo.








0 Comments