Header Ads Widget

MCHEZO WA NGUMI KUZINDULIWA KESHO ZANZIBAR




Matukio Daima App, Zanzibar.

KUFUATIA Katazo la Muda Muda Mrefu sasa Mchezo wa Ngumi za Kulipwa Zanzibar hapo kesho unakwenda kufunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwingi  katika Viwanja vya Maotsung ambapo leo zaidi ya Mabondia 14 akiwemo Dulla Mbabe na Karimu Mandong wamepima uzito kuelekea mapambano hayo.


Hafla fupi ya Upimaji wa uzito ilifanyika katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Sheikh Abeid Aman Karume, Kisonge Mjini Unguja na kuhudhuriwa na Mamia ya Wananchi Visiwani humu huku Mabondia kila Mmoja aliweza kumtambia mwenziwe kuwa atampiga katika Mapamban hayo.


Vituko mbalimbali vilishuhudiwa huku Karimu Mandonga akiwa kivutio zaidi kutokana na maneno na kauli mbiu yake kuelekea Mapambano hayo.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania Chaurembo Palaso amesema kuwa, ameridhishwa na hamasa ya Mchezo wa Ngumi visiwani Zanzibar huku akitarajia kuona burudani zaidi.


Nae Afisa Uhusiano wa Tosh Sport Matlida Peter amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia zote kinachosubiriwa ni mapambano tu.


Amesema katika Usiku wa Masumbwi Zanzibar utasinddikizwa na Burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii kama vile Ali Kiba na Baba levo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI