Header Ads Widget

KAMANDA MUTAFUNGWA, TOKENI OFISINI NENDENI MKATATUE CHANGAMOTO KWA WANANCHI

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA 

MWANZA, Wakuu wa polisi wa Wilaya, Wakuu wa vituo, Maafisa polisi jamii ngazi ya Mkoa, Wilaya, na wakaguzi wa kata wametakiwa kuachia ofisi na kwenda kwenye maeneo ya kata kwa ajili ya kufanya mikutano na wananchi inayolenga kuzuia, kudhibiti uhalifu na kutatua changamoto mbalimbali za kiusalama katika maeneo yao ya kazi.

Rai hiyo imetolewa leo jumanne Aprili 29, 2026 na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya kumpongeza Koplo Stella Lyimo ambaye ni mtendaji wa dawati la jinsia na watoto Wilaya ya nyamagana aliyepata tuzo ya mwanamke kinara katika kipengere cha ustawi wa jamii ambapo alitajwa kufanya vizuri katika kutoa elimu ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa jamii.

Mutafungwa amesema  askari polisi wanawajibu wa kuwajibika ipasavyo katika maeneo yao ya kazi kwa kuwahudumia wananchi kwa kulinda raia na mali zao, lengo ni  kuwa na taasisi ambayo inaheshimika na kupendwa na wananchi

"Kwa wakaguzi wa kata hamieni kwenye kata zenu mkatimize wajibu wenu wa kufanya mikutano na wananchi, zungumzeni na makundi mbalimbali ili mfahamu migogoro iliyopo ndani ya familia ili kuhakikisha mnatatua migogoro hiyo kabla haijaleta madhara"Alisema Mutafungwa.


Jeshi la polisi linadhamana kubwa ya kuhakikisha linatoa huduma kwa wananchi wakati wote, hivyo askari wote tuendelee kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia kazi tunazozifanya.

"Nawahimiza watendaji wote kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia nidhamu uadilifu, uwajibikaji pamoja na haki kwa wananchi" Alisema Mutafungwa

Aidha ameeleza kuwa matukio ya mauji yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali ya mitaa wanao uwezo wa kuyazuia kwani mauaji mengine yanasabishwa na migogoro ya ardhi ya muda mrefu, imani potofu za kishirikina.

"Nendeni mkaingilie kati, kwa kuwapa elimu kwani kwa  kufanya hivyo mtakuwa mmebadilisha makundi kwenye familia na jamii hatua itakayosaidia vitendo hivyo kumalizika" Alisema Mutafungwa.

Kwa upande wake Mkaguzi kata wa kata ya mabatini iliyoko Wilaya ya Nyamagana Mkoani hapa Shabani Kashakala amesema maelekezo yaliyotolewa na kamanda Mutafungwa ameyapokea na kuahidi kuyatekeleza kikamilifu.

Kashakala ameeleza kuwa wanapokuwa karibu na jamii wanapata fursa ya kufahamu migogoro inayoendelea ikiwemo ya kifamilia, Ardhi pamoja na yawafugaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI