Header Ads Widget

MAOFISA MIPANGO NA WAKUU WA VITENGO VYA IT WATAKIWA KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

 



NA THABIT MADAI,ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP


MAOFISA mipango na wakuu wa vitengo vya habari na Mawasiliano (IT) wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wametakiwa kushirikiana pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuiwezesha serikali kufikia malengo ya mabadiliko ya TEHAMA.  


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa serikali Mtandao Said Seif Said wakati akifungua kikao cha kujadili rasimu ya sera ya serikali mtandao (E Government Policy) na mpango mkakati wa serikali mtandao (e Government Strategic Planning) ulioshirikisha wakurugenzi wa Mipango na IT kutoka serikalini kilichofanyika katika ukumbi wa Shekh Idrissa Abdul Wakili Kikwajuni.


Alisema ni lazima kwa watendaji hao kufanya kazi kwa karibu kwani ili mambo yamweze kufanikishwa masuala ya IT sio tena katika kufanya program bali ni kujua wanapoanza, walipo na wanapofikia.    


Aidha alibainisha kuwa watu wa mipango watasaidia kuifikisha serikali inapotaka kufika kuibadilisha Zanzibar kuwa ya kidigitali.


Mkurugenzi Said alisema teknologia hivi sasa zinabadilika hivyo ni lazima kuziangalia kwa karibu ili waweze kufaiidika nazo na waweze kufika wanapotaka kufika.


"Lengo la serikali mtandao ni kuona tunashirikiana pamoja ili kuona tunafika pale tunapotaka na hii sera sio ya wakala pekee bali ni ya serikali nzima kuona tunafika pale tunapopataka na kufikia malengo ya serikali wanayoyataka," alisema.


Hata hivyo, alisema azma ya serikali ni kuhakikisha wanatumia Tenkologia ya Habari na Mawasiliano katika utendaji wa serikali kuona unabadilika na unakuwa kidigitali na huduma za umma zinatolewa kwa urahisi na ufanisi mkubwa popote walipo.


Alifahamisha kuwa ni lazima watendaji hao kufahamu muelekeo wa serikali na kufikia pale wanapotakiwa kama malengo ya serikali yanavyoonesha.


"Mwezi uliopita tulizindua uchumi wa kidijitali wa 2023 hadi 2027,Julai 29 Rais Mwinyi amezindua mkakati wa serikali kidijitali yote haya yakiwa na malengo ya kuhakikisha kwamba TEHAMA haiwezi kuepukika bali itasaidia kufika mbele na wananchi wa Zanzibar kufaidika," alibainisha    


Sambamba na hayo alisema utumiaji wa TEHAMA kwa Zanzibar yana umuhimu mkubwa kwani Zanzibar ni ya mwanzo kwa Afrika kuona huduma zinafanywa kwa ubora zaidi hasa kwa wageni wanaokuja nchini.


Aliahidi kuwa serikali kupitia E -Goverment itakikisha inaendelea kuilinda mifumo hiyo na haichezewi na inaleta tija katika uchumi wa nchi.


Mwenyekiti wa Bodi wa Ushauri E- Goverment, Dk.Mzee Suleiman Mndewa, alisema wameanza safari ya mabadiliko hivyo ni lazima kuwa na miongozo ambayo itasaidia katika kuleta mabadiliko ya Tehama nchini.


Alisema imefika wakati sasa kwa watu wa IT wasilale kwani hawapo vizuri katika kujiongeza kielimu.


"IT tupo 800 lakini kiwango chao  cha elimu sio cha kuridhisha kati yao 25 ndio wana digirii na waliobaki wote wanacheti na diploma," alisema.


Hivyo, aliishauri wakala huo kupitia wizara yake ni lazima Chuo cha IPA kupeleka mitaala ambayo itaweza kuinua kiwango cha elimu kwa wafanyakazi wa IT.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI