Header Ads Widget

MAFURIKO YAUA 49 INDIA


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, India.

Takribani watu 49 wamefariki na katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Nepal na wengine 17 wakifariki huko India kutokana na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya nchi hizo, tisa kati yao wamepoteza maisha kufuatia kuporomoka kwa hekalu la ibada nchini humo.


Watu wengine chungu nzima wakihofiwa hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko na maporomoka ya ardhi. Watu 41 wamepoteza maisha ndani ya kipindi cha masaa 24 katika mkoa wa Himachal Pradesh.Mvua za siku kadhaa zimesababisha mafuriko yaliyosomba magari, majumba kuporomoka na kuvunjika kwa madaraja katika majimbo ya kaskazini ya Uttarakhand na Himachal Pradesh. 


Hali ya mafuriko na maporomoko ya ardhi sio kitu kigeni katika maeneo hayo na husababisha uharibifu mkubwa katika msimu wa masika lakini wataalamu wanasema mabadiliko ya tabia nchi yameongeza kasi ya hali hiyo pamoja na athari.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI