Header Ads Widget

KATA ZA ARUSHA CHINI NA MABOGINI KUFIKIWA NA MIRADI YA REA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

WANANCHI wa vijiji vya Mikocheni ndogo, Chemchem na Chemchem shuleni katika kata ya Arusha chini Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wanaenda kuondokana na adha ya nishati ya umeme baada ya kampuni ya Ok Electrical Service LTD kupewa tenda ya kupeleka umeme katika maeneo hayo.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Prof Patrick Ndakidemi imesema kuwa Mkandarasi huyo yupo kazini kwa ajili ya kusambaza nguzo kwenye maeneo hayo na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwake 


Aidha taarifa hiyo imesema kuwa, kampuni ya Dieynem Company Limited itatekeleza mradi wa kusambaza umeme katika kata  ya Mabogini katika vijiji vya Mtakuja TRF 1, Shabaha, Mtakuja TRF 2 na Upareni.


Alisema kuwa, Mkandarasi huyo ameshafika kuyaona maeneo ya mradi na anajipanga kuanza kazi hiyo na tayari ameshajitambulisha katika kata na vijiji husika.


Kwa upande wao, wananchi wamemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo Prof Patrick Ndakidemi kwa jinsi ambavyo amekuwa akipambana kuhakikisha kero zinazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi.


Amina Rashidi mkazi wa Shabaha alisema kuwa, kupatikana na huduma hiyo ya umeme utachangia kukuza maendeleo ya kata ya Mabogini.

"Tunampongeza sana Mbunge kwa kazi kubwa anazofanya ya kuhakikisha matatizo yanayotukabili yanapatiwa ufumbuzi na sisi tunamuahidi umeme huu tutautumia kujinufaisha katika maendeleo.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI