Header Ads Widget

JAMII IMETAKIWA KUONA UMUHIMU WA KUTUNZA NA KUENZI TAMADUNI ZAO

 



Na, Jusline Marco; Arusha



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Arusha Bw. Ojung'u Salekwa amesema kuwa kutokana na changamoto za maisha ya sasa zinazosababisha watoto wengi kupata malezi ya wasaidizi wa kazi za ndani, suala la utamaduni katika ya jamii umeanza kupotea.




Bw. Ojung'u ameyasema hayo katika Tamasha la Utamaduni lililoandaliwa na Uongozi wa Shule ya Awali na Msingi ya Shepherds Arusha ambapo amesema utamaduni ni kitambulisho cha mtu yeyote hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuendeleza utamaduni wa kabila lake kwa maslahi mapana ya nchi na kuwa na vijana wenye maadili.



Aidha amesema yapo makabila zaidi ya 120 nchini ambayo Mwasisi wa Taifa hili hayati Mwl. Julius Nyerere aliyaunganisha kwa lugha ya Kiswahili na kusema kuwa ni jambo jema kwa mtoto kufahamu utamaduni wa kwao, lugha hata mavazi na chakula chao cha asili.



Amesema kuwa lugha za kigeni na utandawazi vimechangia kwa kiwango kikubwa kuupoteza utamaduni wa mtanzania ambapo amesema kuwa kwa miaka baadae vyakula vya asili vya makabila ya kitanzania vitapotea kutokana na ukuaji wa teknolojia.



Ameongeza kwa kuupongeza uongozi wa shule ya Shepherds kwa kuweza kuandaa tamasha hilo ambalo litawajengea watoto misingi bora na imara katika malezi na maadili mazuri.




Naye Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi Mch. Witness Nadeit ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo amesema suala la utamaduni ni jambo muhimu kwenye maisha katika familia na jami, ambapo amewataka wazazi kuanza kuwafundisha watoto wao utamaduni katika ngazi ya familia kwani ndiyo utambulisho wa kila mmoja.



Ameongeza kuwa utamaduni umebeba mavazi lakini nyakati hizi mavazi yameingia dosari kwa vijana kwa sababu ya utandawazi kwa kuiga mambo mbalimbali kutoka kwenye mataifa mengine bila kujua wanaiga mavazi ya aina gani na hayimaye kuangukia kwenye mmomonyoko wa maadili kwa mavazi yasiyofaa. 



Awali akizungumza wakati wa ufunguzi katika Tamasha hilo Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Shule za Shepherds, Arusha Bi .Lucy Kampton amesema kuwa utamaduni wa mtu yeyote ndiyo kitu pekee kinachoweza kumtambulisha kwani Utamaduni huwaweka watu pamoja na hujenga heshima, upendo na kujenga jamii yenye ubunifu. 



Amebainisha kuwa kutokana na baadhi ya makabila kuishi mijini na kusahau umuhimu wa kuendeleza tamaduni zao, Shule za Shepherds  zimeona haja ya kufanya Tamasha la Utamaduni ili kuwajenga watoto katika kuthamini na kuenzi tamaduni zao mbapo aliwasisitiza wazazi juu ya kutimiza wajibu wa kutunza maadili na kuenzi utamaduni wao katika kujenga kizazi chenye maadili.



Kwa upande wake  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Mwl. Elisha Kayagwa amesema kuwa suala hilo litakuwa endelevu ili kuweza kuwajengea watoto maadili mema kuanzia tabia, malezi na uvaaji. 




"Kupitia siku kama hii ya kuenzi tamaduni zetu, watoto watajua mila na tamaduni zao na za wengine na kuzienzi ninayoa woto kwa wazazi kuendelea kuwafundisha watoto umuhimu wa kuvaa mavazi yenye staha."Asisitiza Mwl.Kayangwa Mkuu wa Shule 



Hata hivyo tamasha hilo la Uyamaduni lilihitimishwa kwa washiriki wote kupata vyakula vya asili vya makabila mbalimbali sambamba na kuchenza ngoma za asili za makabila yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI