Header Ads Widget

EWURA YAWAITA WANANCHI KUPATA UFAFANUZI JUU YA MASWALI YANAYOWATATIZA

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


Na MAONESHO ya Wakulima na wafugaji Kanda ya Kati yamefunguliwa rasmi katika viwanja vya Nzuguni nanenane Dodoma Huku Meneja Kanda ya Kati kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na  Maji EWURA  Hawa Shani Lweno akiwataka wananchi na wadau wote kufika katika banda lao ili kuweza kupata elimu juu ya kazi zinazofanywa  na Mamlaka hiyo.


Akiongea na Matukio Daima Blog Meneja huyo Amesema EWURA imekuwa ikisimimia huduma katika Sekta ya Nishati,mafuta ,Gesi asilia Umeme na Maji.


Aidha amesema Ewura pia imekuwa ikitoa leseni na kazi kubwa na  Msingi ni kusimamia hizo leseni ili Wananchi wote waweze kupata huduma katika ubora zaidi na kuongeza ufanisi katika Mamlaka zote wanazozisimamia Kama EWURA.


Aidha Meneja huyo ametoa wito kwa wakazi na wananchi wote kufika ili kuweza kupatiwa ufafanuzi na kujibiwa maswali yote yalikuwa yakiwatatiza au kujiuliza.


"Kumekuwa na maswali mengi kwa Wananchi juu ya shughuli zinazofanywa na Mamlaka yetu hivyo ili kuweza kujibiwa maswali yote karibuni katika Banda letu kujibiwa maswali yenu , " Amesema Meneja huyo Hawa


Hata hivyo katika Maonesho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni Msingi  imara wa Mifumo endelevu ya Chakula"



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI