Header Ads Widget

ALIYEKUWA DC MBARALI REUBEN MFUNE AACHIWA HURU

 


Na HADIJA OMARY LINDI.....


Mahakama ya wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Reuben Mfune na mwenzake waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi


Uamuzi huo umetolewa Leo August 3, 2023 na hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Mariamu Mchomba baada ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) kuielezea mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo


Inadaiwa kuwa Reuben Mfune na mwenzake walikuwa wanakabiliwa na kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya shilingi Milioni 51 ambapo Katika kipindi hicho Mfune alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kuanzia 2012 - 2015


Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) ameifuta kesi hiyo Kwa NOLLE PROSEQUI chini ya kifungu 91(1) Cha sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai sura ya 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 2022 ambayo iliwasilishwa na wakili wa Serikali mwandamizi Mwanaamina Kombakono



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI