Header Ads Widget

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAONYWA KUHUSU UBADHIRIFU

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 


BARAZA la Ushauri la mkoa Kigoma limepitisha bajeti ya mapato na matumizi kwa mkoa Kigoma ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 270 huku wakurugenzi wa halmashauri za mkoa Kigoma wakionywa dhidi ya ubadhirifu na usimamizi duni wa miradi kwenye halmashauri zao.



Akizungumza baada ya kuwasilishwa kwa  bajeti hiyo Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamali Tamim alisema kuwa bajeti hiyo imelenga kuleta mapinduzi makubwa ya maendeleo mkoani humo na kwamba anaamini bajeti hiyo itatekeleza kwa vitendo mpango  wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati kiuchumi.



Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa Kigoma allisema kuwa kumekuwa na ubadhirifu na matumizi yasiyozingatia niadhamu katika matumizi ya fedha ya utekelezaji wa miradi kwenye ngazi za halmashauri hivyo kuonya wakurugenzi kuwa makini katika kusimamia matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ili kuleta matokeo yanayotarajiwa kwenye miradi hiyo.



Akitoa maoni yake kuhusu bajeti hiyo Mbunge wa jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru alisema kuwa inaenda kuchochea na kuufungua uchumi wa mkoa Kigoma kutokana na miradi ambayo imepitishwa kwenye bajeti hiyo.

 



Pamoja na hivyo Kavejuru alionya kuwa baadhi ya miradi katika bajeri iliyopita imekumbwa na changamoto ya ubadhirifu na utekelezaji kwa viwango duni hivyo kuonya watekelezaji na wasimamizi wa miradi kuwa waadilifu.



Akisoma bajeti hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye alisema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 270 kimepitishwa na bunge na kuwasilishwa kwenye baraza hilo ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 140 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.



Andengenye alisema kuwa fedha hizo ni na zileta mapinduzi makubwa ya maendeleo kwa mkoa huo ambapo hata hivyo ameonya kuwa wingi huo wa fedha hautakuwa na maana kama hakutakuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha na utekelezaji wa miradi iliyopangwa.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI