Matukio Daima, Pwani.
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani imefanya ziara kutembelea vivutio vya utalii na kutambua fursa za uwekezaji Wilaya ya Bagamoyo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji mwenyekiti wa Jwt Abdala Ndauka alisema kuwa baada ya ziara hiyo wameweza kutambua fursa mbalimbali kupitia utalii.
Ndauka alisema kuwa fursa kwa wafanyabiashara ni nyingi sana kwenye utalii pamoja na fursa nyingine kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za utoaji huduma.
"Tumefurahi kutembelea mambo ya utalii tumeona kuna fursa za uwekezaji ikiwa ni pamoja na kutoa huduma zikiwemo za malazi, vyakula na huduma nyinginezo,"alisema Ndauka.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Majid Mhina alisema kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni maeneo mengi yanamilikiwa na watu binafsi.
Naye ofisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Magdalena Kitilla alisema kuwa kuhusu uwekezaji wametenga eneo lenye ukubwa wa hekta 9,800 ambalo linahitaji wawekezaji.
Moja ya wafanyabiashara Fihiri Msangi alisema kuwa ziara hiyo wamejifunza mambo mengi ambayo watayafanyia kazi ili waangalie namna ya kuweza kuwekeza fursa hizo watazitumia vizuri ili kuinua uchumi wa Mkoa huo ambao unategemea uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali na pia unauwekezaji mkubwa wa viwanda.
0 Comments