Na Hadija Omary _Lindi....
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon John (30) mkazi wa mtaa wa Msonobarini Chini kata ya Msinjahili manispaa ya Lindi anadaiwa amejikata uume wake na kisha kukimbilia katika kituo cha polisi wilaya ya Lindi.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mwanaaume huyo ambaye ni mfanyabiashara alifika nyumbani kwake asubuhi majira ya saa 4 asubuhi akitokea kwenye shughuli zake ambapo wanaeleza mara baada ya kuingia ndani kwake walimuona akitoka nje akiwa mtupu na anachuruzika damu sehemu za siri na kuelekea maeneo ya baharini.
Baadhi ya watu ambao walimuona kijana huyo walisema kabla ya kwenda kituo cha polisi alionekana akielekea maeneo ya baharini huku akikimbia akiwa mtupu ameshikilia nguo zake pamoja na pasi ya umeme na damu nyingi zikiwa zinamchuluzika ambapo wanadhani alikuwa na lengo la kujikausha damu
Hata hivyo jambo la kushangaza majirani hao wanasema licha ya tukio hilo kudaiwa kutendeka ndani ya chumba chake lakini walipoingia chumbani humu hawakuweza kuona kitu chenye ncha kali kama kisu au panga chenye kuloa damu ndani ya chumba hiko wala kipande cha uume kilichotolewa
Baadhi ya watu wanasema kwa hali aliyoonekana nayo kijana huyo kuwa uwenda amerukwa na wazimu.
Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Sokoine Dkt Baraka Steven Mshango amekiri kumpokea mwanaume huyo majira ya saa 4:30 asubuhi akiwa na majeraha katika sehemu zake za siri na uume wake ukiwa umeondolewa kabisa.
Amesema baada ya kupokelewa taratibu za matibabu zilianza na kwakua alikuwa anatokwa na damu nyingi na kwa sasa amelazwa katika wodi ya uangalizi maalum.
Mpaka sasa chanzo cha kujikata uume wake hakijafahamika lakini Matukio daima inaendelea na jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi kujua chanzo cha tukio hili.
0 Comments