Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kwenye Mnara unaojengwa katika Mji wa Mtumba Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa,shughuli iliyoambatana na kuweka mchanga wa ujenzi huku akibainisha furaha yake maadhimisho hayo kufanyikia viwanja vya mashujaa Mtumba
Rais Dkt.Samia ameyasema hayo mapema leo Jijini Dodoma kwenye Maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa,kusaini kitabu maalum cha maombelezo ya mashujaa na kupigwa kwa mizinga miwili, ambapo kulifuatia hali ya ukimya kwa dakika moja.
Rais amesema kukamilika kwa uwanja huo wa mashujaa utaendelea kuongeza heshima na hadhi ya makao makuu ya nchi.
"Niwashukuru ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na majeshi yetu kwa maadalizi mazuri ya maadhimisho haya na kusimamia vizuri awamu ya kwanza ya ujenzi wa awamu hii na mnara ," Amesema
Na kuongeza"sasa wa ujenzi unaoendelea wa manara wa kudumu kwasababu nimeambiwa mnara uliopo hapa ni manara wa mwaka huu tuu pengine mwakani nitakuja kwenye mnara wa kudumu ambao ujenzi wake unaendelea”Amesema Rais Dk.Samia.
Aidha ametoa wito kwa watanzania kuwaenzi mashujaa wetu wote kwa kudumisha amani ,umoja ,mshikamano na utulivu wa nchi yetu na kufanya kazi kwa bidi kwaajili ya maendeleo ya taifa letu, kamwe tuskubali mtu yeyote au kikundi cha watu kutugawa kwa kisingizio chocote kile ,Tanzania ni moja na kamwe haitagawanyika.
"Kwa mamlaka naliyonayo aliwaomba waudhuriaji wa shughuli hiyo nkusimama kimya kwa dakika moja ikiwa jni ishara yakuwaombea waliotangulia mbele ya haki kutojkana na kuipigania nchi," amesema Rais Dkt,Samia.
Hata hivyo Amesema kabla haijaanza shughuli hiyo alipofika nilionyeshwa ramani ya namna ya uwanja huu utakavyokua .
"Nimevutiwa sana na ramani ya uwanja wa mashujaa ,uwanja huu utakua na migahawa ya kimataifa ,utakua na kumbi za mikutano, utakua na vivutio vingine vya watu kupumzika na kupata burudani kama michoro ilivyoonyesha kubwa zaidi zaidi utakua na mnara mrefu kabisa ndani ya Afrika yetu kabla ujengwe mwingine kabla wetu haujakamilika lakini kama wetu utakamilika mwanzo utakua na sifa hizo za kuwa mnara mrefu kabisa ndani ya Afrika," Amesema
"Hivyo basi nitumie fursa hii kuielekeza ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na ofisi zingine wote kuendelea kusimamia kwa karibu ujenzi wa mnara pamoja na ujenzi wa uwanja wa mashujaa pamoja na miundombinu mingine yote ikamilike kwa wakati na kwa viwango viliovyokusudiwa, vilevile wizara ya fedha ihakikishe kwamba inatoa fedha kwakuzingati mpangokazi wa ujenzi huu na kusiwe na ucheleweshwaji wowote, " Amesema
0 Comments