Header Ads Widget

PROF. PATRICK NDAKIDEMI "SERIKALI IMETOA BILIONI 5.5 KWA AJILI YA MIRADI MBALIMBALI KATIKA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI"

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MBUNGE wa JImbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi amesema kuwa, jumla ya fedha Bilioni 5.5 imetolewa na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo hilo.


Prof. Ndakidemi alitoa kauli jana wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Old Moshi magharibi ambapo alisema kuwa, fedha hizo zimeelekezwa katika sekta ya miundombinu ya barabara, Elimu, maji, Kilimo na mikopo kwa makundi maalum.



"Serikali imeonyesha kutujali sisi wananchi kwa kutuletea fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sisi jukumu letu ni kuhakikisha tunailinda na kuitunza miradi hiyo ili iweze kudumu" alisema Prof. Ndakidemi.

 
Mbunge huyo aliwashauri wazazi kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuiendeleza shule ya Sekondari ya Kata ya Maringeni ambayo inahudumia watoto wao. 



Katika mkutano huo, wananchi walipata fursa ya kutoa kero zao kwa Mbunge ambapo kero kubwa iliyosemwa na wachangiaji wengi ni ubovu wa barabara kuu inayoanzia Tela Mande hadi Maideni. 


Mwakilishi wa TARURA aliyehudhuria katika mkutano huo aliwathibitishia wananchi kuwa barabara hiyo imetengewa fedha mwaka huu, na itakatabatiwa kwa kiwango cha changarawe.


Kero nyingine ilihusu uchakavu wa Shule ya Msingi Maringeni ambayo haijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu ambapo Mbunge aliwaahidi kuwa kero zote zilizoibuliwa katika mkutano wake atazipeleka Serikalini  ili zipate ufumbuzi.


Katika hatua nyingine Prof. Ndakidemi alipata fursa ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Kata ya Old Moshi Magharibi ambapo aliambatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Ndugu Ramadhani Samweli Mahanyu, madiwani wa Viti Maalum kutoka Tarafa za Hai Mashariki na Kibosho, viongozi wa CCM Kata na matawi kutoka Oldmoshi Magharibi na watendaji wa idara mbalimbali toka Serikalini.



Mbunge alikagua ujenzi wa Maabara inayojengwa katika Shule ya Sekondari  Maringeni ambapo Serikali imeshatoa jumla ya shilingi milioni 30, akiwa hapo shuleni, Mbunge alikagua ujenzi wa choo cha hosteli ya wasichana na nyumba ya kulala ya mwalimu mkuu. 


Pia aliongea na wanafunzi na waalimu na  kuwakaribisha kuja kumtembelea bungeni.  


Mbunge aliendelea na ziara na kufanya ukaguzi wa ujenzi wa Choo cha Ofisi ya kijiji cha Mande ambapo jumla ya shilingi milioni  3 zilito

lewa na Mbunge  kupitia mfuko wa Jimbo.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI