NA HADIJA OMARY _LINDI.....
Benki ya NMB tawi la Nachingwea Mkoani Lindi imekabidhi Magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 4,500,000 katika zahanati ya kambi ya jeshi la kujenga taifa (JKT) 843 KJ Wilayani Nachingwea.
Akizungumza wakati wa ghafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Zahanati hiyo Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kusini Bi. Faraja Ng'ingo amesema vifaa hivyo walivyokabidhi ni moja ya ushirikiano wao katika maendeleo ya jamii ambapo wao kama Benki wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.
Alisema kwa miaka kadhaa sasa Benki hiyo imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi katika sekta ya Elimu, Afya na kusaidia majanga yanayoipata Nchi.
Hata hivyo ng'ingo aliongeza kuwa kama sehemu ya uwajibikaji na kurejesha kwa jamii Benki hiyo imekuwa imekuwa msatari wa mbele kuchangia huduma za jamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida kwa jamii hiyo ambapo kwa zaidi ya miaka saba sasa mfululizo imekuwa ikitenga asilimia 1% ya faida hiyo.
Ng'ingo alisema kuwa wao kama Benki wanatambua juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia za kusimamia upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizi mijini na vijijini.
"Pamoja na makubwa yanayofanywa na Serikali, sisi kama wadau tunaowajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii zetu kwani jamii hizi ndio zimeifanya bank ya NMB kuwa hapa ilipo na kubwq kuliko Banki yoyote hapa Nchini"
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea Adinani Mpyasile alisema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki hiyo katika maswala mbalimbali ya kijamii ambapo amewataka Wananchi wa Nachingwea kuendelea kuitumia benki hiyo ili kudumisha mashirikiano waliyonayo.
Alisema serikali haiwezi kuondoa changamoto zote kwa mara moja hivyo msaada huo uliotolewa unaendelea kuisaidia Serikali katika kuendelea kutatua changamoto mbali mbali za Wananchi wake.
Nae kamanda wa kikosi JKT 843 Nachingwea Luten Canal Nyagalu Malecela aliwashukuru NMB kwa msaada walioutoa ambapo amesema kuwa Magodoro hayo licha ya kuwasaidia watu wanaoishi katika kambi hiyo lakini pia yatawanufaisha pia Wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo ambao wanapata huduma za Afya katika zahanati hiyo.
0 Comments