Header Ads Widget

LUHANJO: UTALII UTANGAZWE KWA KUTUMIA SANAA YA FILAMU TANZANIA

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati taifa likitegemea vyanzo vya maji vilivyopo katika mkoa  wa Njombe kuzalisha Umeme ,Kikundi cha filamu cha Sinai kilichopo Ilembula wilayani Wanging'ombe  kimezindua filamu inayohamasisha utalii na uhifadhi wa mazingira katika hifadhi ya Mpanga Kipengere.


Akisoma taarifa ya mradi huo wa kutangaza utalii kupitia pori la akiba la Mpanga kipengere Antony Mlowe anasema wamefanikiwa kuandaa filamu hiyo itakayosaidia kutangaza na kukuza utalii kusini mwa Tanzania huku Mwenyekiti wa kikundi hicho Godfrey Nyagenda akisema sanaa ina nafasi kubwa ya kutangaza vivutio.



Meneja wa pori la akiba la Mpanga kipengere Donasian Makoi amesema mpango wa kukuza na kutangaza utalii katika hifadhi hiyo kutokana umuhimu wake mkubwa umekuja kwa kuwa ni msaada mkubwa katika kupeleka maji kwenye mito mitatu mikubwa inayozalisha umeme kwa nchi nzima  kauli iliyoungwa mkono na Alphonce Mng'ong'o afisa wanyamapori mkuu.


Mlezi wa kikundi cha Filamu cha Sinai Mzee Danford Mpumilwa ambaye ni mwanahabari mstaafu anatumia fursa hiyo kuiomba serikali kuviwezesha vikundi vinavyofanya shughuli za kutangaza utalii ili viweze kufanya kazi nzuri zaidi.



Anitha Kivike ni afisa michezo utamaduni na sanaa Wilaya ya Wanging'ombe ambaye amesema Watanzania wanapaswa kuanza kutembelea vivutio vya ndani Kwanza ndipo watoke nje kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya kutotembelea vivutio vya ndani.



Kwa Upande wake katibu mkuu kiongozi mstaafu mzee Philimon Luhanjo wakati akizindua filamu hiyo ameitaka Wizara ya maliasili na utalii  kuona umuhimu wa kuvitumia vikundi Kama Cha Sinai katika kutangaza utalii Kitaifa na  kimataifa  huku Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta akiwataka wananchi kuhakikisha wanatunza maeneo yote ya hifadhi bila kuyaingilia ili yaweze kulinufaisha taifa.


Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan alizindua filamu maalum ya kutangaza vivutio vya utalii ya Tanzania The Royal Tour na kuahidi kuendeleza mpango huo katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI