Header Ads Widget

MBUNGE PROF NDAKIDEMI AFANYA ZIARA OLD MOSHI MAGHARIBI

 Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI

Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro  Profesa Patrick Ndakidemi   ameanza ziara ya kutembelea jimbo lake la    kwa kutembelea kata ya Old Moshi Magharibi, Vijiji vya Tela na Mande.

Ziara hiyo imeanza kwa kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika kata ya Old Moshi Magharibi.

Katika hatua ambayo inaonekana kuwa na mafanikio zaidi pia  ameambatana na katibu wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini  Ramadhani  Mahanyu, madiwani wa Viti Maalum kutoka Tarafa za Hai Mashariki na Kibosho, viongozi wa CCM Kata na matawi kutoka Oldmoshi Magharibi na watendaji wa idara mbalimbali toka Serikalini.

Hapo ndipo mbunge akaanza ziara kwa kukagua ujenzi wa aabara inayojengwa katika Shule ya sekondari  Maringeni ambapo serikali imeshatoa jumla ya shilingi milioni 30. 

Akiwa hapo shuleni,  amekagua ujenzi wa choo cha hosteli ya wasichana na nyumba ya kulala ya mwalimu mkuu ila  kabla ya kuondoka shuleni, Mbunge aliongea na wanafunzi na waalimu.

Pia  amewakaribisha  kumtembelea bungeni na hatimaye  kuendelea na ziara na kufanya ukaguzi wa ujenzi wa choo cha ofisi ya kijiji cha Mande ambapo jumla ya shilingi milioni  3 zilitolewa na mbunge  kupitia mfuko wa jimbo.

Katika mkutano wa hadhara MheProf Ndakidemi  amewaeleza wananchi wa Kata hiyo idadi ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa ambapo jumla ya shilingi Bilioni  5.5 zimeshaelekezwa katika miradi ya maendeleo kwenye  sekta za miundombinu ya barabara, elimu, maji, kilimo na mikopo kwa makundi maalumu.

Sasa hapa ndipo  mbunge anawashauri wazazi kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuiendeleza shule ya sekondari ya kata ya Maringeni ambayo inahudumia watoto wao. 

Katika mkutano huo, wananchi walipata fursa ya kutoa kero zao  zikiwemo zile ambazo zimesemwa na wananchi walio wengi kuwa ni ubovu wa barabara kuu inayoanzia Tela Mande hadi Maideni.

'Bara baraza katika hili eneo letu bado ni tatizo sugu na kuwa linachangia kukwama Kwa shughuli za maendeleo na kama tukipata ufumbuzi huenda tukawa mbali kiuchumi zaidi ya hapa'anasema Gerson Onesmo

 Mwakilishi wa TARURA aliyehudhuria katika mkutano huo(hakutaka kutaja jina Kwa kuwa sii msemaji) amewathibitishia wananchi kuwa barabara hiyo imetengewa fedha mwaka huu, na itakatabatiwa kwa kiwango cha changarawe.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI