Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MKURUNGEZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt Jabir Bakari amesema Takwimu zinaonesha kuongezeka kwa asilimia 17 ya watumiaji wa Intaneti Kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kutoka watumiaji
29,169,958,mwezi Julai 2022 hadi kufikia 34,045,384mwezi Juni 2023.
Hayo Amebainisha leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa utekelezaji wake kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Mkurugenzi huyo amesema Sababu kuu
zinazochangia ongezeko la matumizi ya intaneti ni uwepo wa maudhui
ya Kiswahili kwenye intaneti ikijumuisha kuongezeka kwa Program tumizi (applications) kwa lugha ya Kiswahili.
"Wastani wa Bei za Data (Tshs)
Mwenendo wa gharama za rejareja za data bila kifurushi na kwenye kifurushi kuanzia 2015 –Juni 2023 (ikijumuisha kodi) zimeendelea kupungua na kuongeza utumiaji wa huduma
za Intaneti nchini kama inavyoonekana hapa chini," Amesema Mkurungezi huyo Dkt Bakari
Katika hatua nyingine Dkt Bakari ameeleza kuwa takwimu zinaonyesha kwamba mikoa mitano (5) Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika yaani (Active SIM-cards) ikiwemo Dar es Salaam (Laini Milioni 11,797,544), Mwanza (Laini 4,246,212), Arusha (3,858,283), Mbeya (3,687,622) na Dodoma (3,421,006).
ambapo Amesema Gharama za Muunganisho wa simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimekuwa
zikipungua mwaka hadi mwaka.
Amesema Mwaka 2015 gharama zilikua ni TZS 30.58na kwa sasa
gharama zilizokokotolewa ni TZS 1.86kwa dakika.
"Hii inachangia kupunguza gharama za
rejareja za upigaji wa simu na kuondoa ulazima wa wateja kuwa na simu zaidi ya moja," Amesema Mkurungezi huyo Dkt Bakari
Aidha Mkurungezi huyo amesema Katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Juni 2023 TCRA imefanya utafiti na kupelekea kupatikana kwa gharama mpya za mwingiliano wa simu baina ya mitandao kuanzia mwaka 2022 hadi 2027.
Ametaja gharama hizo, ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo zilikuwa TZS 2.00,
zimepungua hadi TZS 1.86 kwa mwaka 2023.
Amesema Mafanikio hayo yamechangia
kupungua kwa gharama za rejareja za upigaji wa simu baina ya mitandao, hivyo Kuondoa ulazima wa wateja kuwa na laini za simu zaidi ya moja.
Hata hivyo Amesema Mamlaka imebaini kuwa mwenendo wa gharama ndani na nje ya Mtandao ndani ya kifurushi zimeendelea kushuka
na kukaribiana hali inayochochea shughuli nyingi za kiuchumi kufanyika kupitia mawasiliano ya simu ukilinganisha na hapo awali.
0 Comments