Header Ads Widget

ZAIDI YA WAJASIRIAMALI 800 KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA VIWANDA NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati shirika linalohudumia viwanda vidogovidogo SIDO Likitarajia kufanya maadhimisho ya viwanda Kitaifa katika mkoa wa Njombe hapo mwezi oktoba mwaka huu Rai imetolewa kwa wajasiriamali mbalimbali kuyatumia maadhimisho hayo kukuza uchumi wao.


Katika mkutano na waandishi wa habari,Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema zaidi ya wajasiriamali 800 toka ndani na nje ya nchi wanatarajia kushiriki katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.


Mkurugenzi mkuu wa SIDO taifa Mhandisi Sylvester Mpanduji amesema katika maadhimisho hayo kutakuwepo na utoaji elimu kwa wajasiriamali ili kupunguza changamoto zilizopo.



Tanzania imetajwa kuwa na upungufu mkubwa wa viwanda vinavyotengeneza vifungashio ambapo Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji SIDO Bi.Shoma Kibende  amesema fursa ya maadhimisho hayo inapaswa kuwafungua watanzania kuwekeza katika viwanda.


Kwa upande wake meneja wa SIDO Mkoa wa Njombe Isdory Kiyenze amesema maadhimisho hayo yatakuwa na tija kubwa kutokana  na fursa zilizopo mkoani Hapa.



Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Ibrahim Lubugo na Nichoraus Luoga wamekiri kuwa ujio wa maadhimisho ya viwanda kitaifa mkoani Njombe yatakuwa ni fursa kubwa kwao kwani watafanya biashara za vyakula,usafirishaji na hata nyumba za kulala wageni achilia mbali fursa za ujasiriamali wa Kiviwanda.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI