Header Ads Widget

TEKNOLOJIA DUNI CHANGAMOTO UZALISHAJI MAWESE

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Zaidi ya asilimia 60 ya mafuta ya mawese inatajwa kupotea kutokana na dhana duni za uchakataji wa bidhaa hiyo hivyo kupelekea mafuta hayo kuwa katika kiwango cha chini. 

 

Akizungumza na vikundi viwili vya wachakataji wa mafuta ya mawese wakati wa kuwekeana saini mkataba wa awali na vikundi hivyo wa kununua mitambo ya kisasa katika kata ya Bubango Halmashauri ya Wilaya Kigoma Mkurugenzi wa ubunifu wa tume ya Sayansi na teknolojia nchini (COSTECH), Kufuku Gerlad alisema kuwa kutokana na tija ndogo ya uzalishaji wa mafuta ya mawese wamelazimika kuwasidia wakachataji hao ili iweze kufikia asilimia 80. 


Alisema kuwa mkakati wa serikali ni kusimamia zao la chikichi ili kuongeza uzalishaji wa mafuta ya mawese ambao utaongeza upatikanaji wa mafuta ya kula ya kutosha nchini. 

 

“Bado hatujawa na tija kwenye uzalishaji wa mafuta ha mawese ambapo zaidi ya  asilimia 60 ya uzalishaji unapotea wakati wa uchakataji sababu ya zana duni hivyo tunatarajia mpango huu tunaouanzisha utasaidia kuongeza uzalishaji angalau kufikia asilimia 80 ya kiwango cha mafuta ya kula yenye ubora na yanayofaa kwa matumizi ya binadamu"alisema Gerald 



Nae Afisa Maendeleo ya jamii  Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Jabiri Timbuko alisema kuwa mpango wa COSTECH kusaidia utaalam na teknolojia kwa vikundi viwili vya wachakati wa mafuta ya mawese kutoka Kata ya Bubango  utasaidia kuboresha teknolojia ya uchakati na kuongeza uzalishaji wa mawese. 

 

Alisema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya teknolojia duni ya uchakataji halmashauri imetoa wastani wa shilingi milioni 40 kusaidia ununuzi wa mashine ya kuchakataji wa mafuta ya mawese kwa wachakataji wadogo.


Kwa upande wake Katibu wa kikundi cha Wajane  wa Kata ya Bubando Hadija Maulid alisema kuwa wanashindwa kuzalisha mafuta ya kula yenye ubora kutokana na teknolojia duni wanayotumia lakini wanapoteza kiasi kikubwa cha mafuta wakati wa kuchakata hivyo anaamini kuwa kuja kwa COSTECH kutasaidia kukabiliana na hali hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS