Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Jumla ya Watu 1142 wanatarajiwa kuanza kulipwa fidia za kupisha maeneo ya madini ya Chuma na Makaa ya mawe Wilayani Ludewa mkoani Njombe hapo Juni 7 mwaka huu kiasi Cha zaidi shilingi bilioni 15.4.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la maendeleo la taifa NDC Dkt Nicolaus Shombe amesema tayari uhakiki wote ulishafanyika na wanufaika walishakula kiapo hivyo zoezi hilo litazinduliwa rasmi siku ya juma tano ya wiki hii.
Amesema kutakuwepo na shughuli mbalimbali ndani ya miradi hiyo kikiwemo chuo Cha ufundi na hivyo mwakani shughuli za uchimbaji migodi hiyo inatarajiea kuanza.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema uzinduzi huo utafanyika na waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Dkt.Ashatu Kijaji zoezi litakalofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa.
Aidha Mtaka amesema fedha hizo pia zinaweza kuwasaidia kuwekeza katika shughuli nyingine badala ya kwenda kuzitumia vibaya.
0 Comments