Header Ads Widget

RAIA NA ASKARI WAUA SIMBA KIJIJI CHA ILOWELO MBEYA

Na Matukio daima media,  Mbeya

ASKARI wa wanyapori kwa kushirikiana na wananchi Mtaa wa Itezi Magharibi wamefanikiwa kumuua Simba baada ya kuua ng'ombe wawili na punda mmoja Kijiji cha llowelo Kata ya Lwanjilo Wilaya ya Mbeya.

Akizungumza na Matukio daima ,Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilowelo Kata ya Lwanjilo Wilaya ya Mbeya vijijini, Yona  Samweli amesema Simba huyo aliibuka siku sita zilizopita ambapo waliotoa taarifa Maliasili ambapo walifika na kuanza msako.


Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema tukio  hilo ni la tatu kutokea  katika kijiji cha Ilowelo sababu ni mapito ya wanyama kutoka Ruaha kwenda hifadhi ya Katavi.

Amesema kuwa baada ya kugundua anasakwa Simba huyo aliondoka na kuvamia mtaa wa Itezi Magharibi ambapo aliuua punda watatu na ng'ombe mmoja hali iliyotishia kutoweka kwa amani kwa wananchi .

Mwenyekiti wa Mtaa wa Itezi Magharibi, Mario Paul amesema Simba huyo alikuwa tishio kubwa ambapo wananchi hasa watoto wadogo walikosa amani  ambapo walifanikiwa kumuua korongoni wakati akila mzoga wa punda.

Afisa wanyapori Wilaya ya Chunya, Jacob Mpinga amesema baada ya askari kufanikiwa kukabiliana na Simba huyo walifanikiwa kumuua na mwili wake kuchukuliwa na kuhifadhi nyara hiyo ofisi za maliasili.

Amesema hii ni kawaida kwa wanyama kutoka hifadhini wakifuata ushoroba kwenda maeneo mengine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS