Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MTAFITI Mkuu kutoka (TAWIRI) Dkt Hamza Kija Amesema Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori za Jamii (NWMAS: 2023 - 2033) unatoa mwongozo wa kimkakati wa kujenga uelewa na namna ya kukabiliana na changamoto ili kuhakikisha maendeleo endelevu ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori za Jamii (WMAs) nchini Tanzania yanatunzwa.
Akiongea jijini Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wakudhibiti ujangili 2023 Hadi 2033 na mkakati wa usimamizi wa maeneo ya jumuiya za hifadhi za wanyama Dkt Hamza Amesema mkakati huo umeandaliwa kwa kuzingatia fursa na mafanikio ya miaka 5 ya utekelezaji wa mkakati uliopita.
Kija amesema mkakati huo unaendelea kutambua jitihada za Serikali na wadau wengine katika sekta ya wanyamapori na umekusudiwa kuongoza juhudi za usimamizi na maendeleo ya WMAs katika kipindi cha miaka kumi kuanzia 2023 hadi 2033.
"Mkakati huu unalenga kuhakikisha uhifadhi endelevu wa wanyamapori, ulinzi wa makazi yao, na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa Taifa, kuchochea maendeleo endelevu, kukuza utalii (wa picha na uwindaji) na kuboresha ustawi wa jamii zinazoishi karibu na maeneo haya na kijamii. Lengo Kuu," Amesema Dkt Hamza
Na kuongeza"Lengo kuu la Mkakati huu ni kuwezesha WMAs kuwa nguzo muhimu ya uhifadhi wa wanyamapori, kuchochea maendeleo endelevu, na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za wanyamapori nchini,".
Mkakati huu pia unalenga kutoa mwongozo (road map) ili (i) kuongeza faida za dhana ya WMA katika uhifadhi wa rasilimali za asili; na (ii) kupunguza athari hasi zinazohusiana na ongezeko la idadi ya wanyamapori.
MALENGO MAHSUSI YA MKAKATI.
Kuchochea uhifadhi wa wanyamapori na kuhakikisha uhifadhi endelevu wa rasilimali za wanyamapori na makazi yao.Kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, wadau wa uhifadhi, na jamii zinazoishi karibu na WMAs.Kukuza uchumi na maendeleo katika jamii zinazozunguka WMAs kupitia shughuli za utalii na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori.
Kuendeleza mipango ya uhifadhi wa wanyamapori na kuboresha usimamizi wa jumla wa WMAs.Kuongeza uwezo wa kitaasisi na rasilimali watu katika usimamizi wa WMAs.Malengo Mkakati (Strategic Objectives)Kuongeza idadi ya WMA zilizofanikiwa (To scale up the successful WMA model)Kuboresha utawala na mfumo wa usimamizi wa WMAs kwa kufuata taratibu za uendeshaji zilizo na ufanisi wa kiwango cha juu.
Kuimarisha uwezo wa vitengo vya usimamizi na utawala wa WMAs katika kuzingatia malengo ya kijamii na biashara endelevu kwa muda mrefu. Kukuza mifumo ya kifedha na fursa mpya za kiuchumi za WMA zaidi ya utalii (kama biashara ya kaboni) ambazo zinazalisha faida kubwa.
Malengo mengine ni kuweka mazingira salama yanayowezesha sekta binafsi kuwekeza katika WMAs na Kuifanya CWMAC kuwa taasisi imara ya kitaifa inayosimamia muungano wa WMAs (To make CWMAC a stronger community-owned national body)Kuandaa na kusimamia mpango mkakati wa CWMAC wenye ufanisi ambao utaboresha na kuendeleza usimamizi wa WMAs ili kufikia malengo ya kimkakati.
Amesema malengo mengine ni kuweka mfumo endelevu wa kiuchumi kwa CWMAC ili kusaidia shughuli za uhamasishaji za WMAs katika ngazi ya kitaifa, katika usimamizi, utawala wa taasisi, na ulinzi wa rasilimali za asili. Kuweka na kuimarisha mfumo wa habari (za kiikolojia na kiuchumi-kijamii) zitakazokusanywa, kuhifadhiwa, kuchambuliwa, kufuatiliwa, na kushirikisha wadau kwa ajili ya Ufuatiliaji na Tathmini ya utendaji wa WMAs.
Malengo mengine ni Kuendeleza na kuboresha zana na mfumo kwa WMAs na matumizi ya zana hizo ili kuboresha, kufuatilia, na kutathmini utendaji na athari za WMAs kila wakati. Kuendeleza zana na njia za kuimarisha uwezo ili kusaidia WMAs katika vipaumbele vya uwekezaji na mazungumzo ya mikataba pamoja na Kuimarisha mifumo ya sera na sheria rafiki na kuboresha utekelezaji wa kanuni, taratibu na sheria zinazosimamia WMAs (To develop and strengthen supportive policy and legislative frameworks).
0 Comments