Header Ads Widget

MANSOUR ATOA USHAURI KWA SERIKALI

 




NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR - MATUKIO DAIMA APP



MSHAURI wa mwenyekiti wa chama cha ACT WAZALENDO na waziri wa zamani zanzibar Mansour Yusuf Himid amesema hakuna sababu za msingi za barabara ya uwanja wa ndege hadi mnazimmmoja kuvunjwa wakati ilitumia gharama kubwa kufanyiwa matengenezo mwaka 2020.



Mansour ameyasema hayo alipokua akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa paje mkoa wa kusini unguja, uliohudhuriwa na makamu wa kwanza wa rais ambae pia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Othman Masoud Othman.



Amesema inashangaza serikali imevunja barabara nzima badala ya kuvunja na kujenga barabara mbovu bila ya kujali matumizi mabaya ya fedha za umma wakati zanzibar ni nchi masikini.




kwa upande wake mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho, ismail jussa ladhu amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulitawaliwa na vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu baada ya watu 21 kupoteza maisha kwa kupigwa riasasi na wengine kupata ulemavu wa kudumu.




Makamu mwenyekiti wa ng’ome ya wanawake Pavu Juma Abdallah amesema mikopo kupitia fedha za uviko-zimetolewa kwa upendeleo kwa itikadi za kisasa jambo ambalo ni kinyume na misingi ya haki za binadamu.



Chama cha act wazalendo kimeanza mikutano wa hadhara huku wakitumia muda mwingi kukosoa serikali ikiwemo kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa majengo wa huduma za jamii na miradi ya barabara.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI