Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
JESHI la Kujenga Taifa JKT limewataka Wazazi, walezi na Vijana waliopangiwa kuhudhuria mafunzo ya JKT katika makambi mbalimbali kuzipuuzia taarifa zilizisambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa mafunzo ya JKT ni Mateso, yana unyanyasaji na udhalilishaji hususan kwa vijana wa jinsi ya kike.
Mkuu wa tawi la Utawala Jeshi JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena ametoa tamko hilo melitoa Leo jijini Dodoma wakati Akiongea na waandishi wa habari wakati ambapo amesema taarifa hizo ni zauzushi na hazina ukweli wowote kwani mafunzo hayo ni muhimu kwa ustawi wao na Taifa kwa ujumla.
Aidha amesema Jeshi la JKT linapenda kuutarifu Umma kuwa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria na yale ya kujitolea yanalenga kumjenga Kijana wa kitanzania uzalendo ,ukakamavu, nidhamu na kuleta umoja wa kitaifa.
" Mafunzo yaha yanaedeshwa kwa kuzingatia Mila, desturi na tamaduni za kitanzania kwa kufuata silabi ya mafunzo na miongozo ya maelezi ya vijana inayotolewa na makao makuu ya JKT, " Amesema Brigedia Mabena.
Na kuongeza" Vijana wanapokuwa makambini muda wote wa mafunzo wanakuwa chini ya uangalizi wa wakufunzi wao ambao Wana weledi na uzoefu wa kuendesha mafunzo haya , kwa kuwa wameoewa dhamana ya kuhakikisha Taifa linapata vijana wazalendo, wenye nidhamu na ukakamavu, watakaokuwa tayari kulilinda na kulitumikia Taifa lao, " Amesema Brigedia huyo.
Amesema katika kuhakisha vijana hao wanakuwa salama wakati wote makambi na vikosi vyote vya JKT vina baba na mama mlezi ( Patron na Matron) ambao wamewekwa mahususi ili kusimamia ustawi was vijana wa kiume na wakike kwa Kipindi chote wanapokuwa makambini.
"Na endapo ikabainika kunaufafanuzi anakwenda kinyume na Sheria na taratibu zilizowekwa za miongozo ya maelezi ya vijana ndani ya JKT, hatua kali za kinidhamu na kisheria zinachukuliwa dhidi yake,"amesema Brigedia Mabena.
Hata hivyo JKT linatoa rai kwa Umma wa watanzania kuwa mtu yoyote mwenye nia ovu ya kueneza taarifa za uzishi na uongo zinazohusu JKT katika mitandao ya kijamii ikibanika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hilo Brigedia Mabena amesema Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele anapenda kuwatoa hofu wazizi walezi na vijana walioitwa kuudhuria mafunzo ya JKT kuripoti katika makambi walioteuliwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.
" Mafunzo haya Wala haya lengi Kutoa manyanyaso kutesa au kudhalilisha vijana hivyo basi vijana wote walioteuliwa kuudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu sheria kwa mwaka 2023 ," Amesema.
0 Comments