Header Ads Widget

JENGO LA MADUKA LINALOMILIKIWA NA UWT SHINYANGA (JJ) LATEKETEA KWA MOTO




Mali za Wafanyabiashara wapatao 10 ambazo thamani yake bado haijajulikana, zimeteketea kwa moto ulitokea usiku wa kuamkia leo Juni 6, 2023 katika jengo la maduka linalomilikiwa na Umoja wa Wanawake Tanzania UWT mkoa wa Shinyanga, maarufu kama JJ, lilipo mkabala na ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Shinyanga.


Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, moto huo umeanza majira ya saa nane usiku na kusababisha vyumba saba  vya maduka kuungua huku sita vikiokolewa.



Wakizungumza kwa masikitiko makubwa, baadhi ya wafanyabishara waliopoteza mali zao, wamesema walipigiwa simu usiku na mlinzi wakijulishwa kuhusu maduka yao kuteketea kwa moto, ambapo walitoa taarifa kwa Jeshi la zima moto na kufika kujaribu kuuzima moto huo, baada ya magari ya Jeshi hilo kuchelewa kufika katika eneo la tukio.


Akizungumzia tukio hilo Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Bi. Asha Kitandala, amesema tukio hilo limewarudhisha nyuma Wafanyabishara waliokuwa wakifanyia biashara katika jengo hilo na kwamba, UWT pia walikuwa wakilitegemea kwa mapato.



Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, ingawa taarifa za awali zinaeleza kuwa,umetokana na hitilafu ya umeme.


Juhudi za kulipata Jeshi la zimamoto kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.



CHANZO: MALUNDEBLOG

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS