Header Ads Widget

DC KAGANDA ASAS ZA KIRAIA KUWEKA WAZI TAARIFA ZA FEDHA TOKA KWA WAHISANI

 


Na,Jusline Marco ,Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Emmanuela  Kaganda ameyataka Mashirika yasiyo ya kiserikali kuweka wazi taarifa zao za mapato na matumizi ya fedha toka kwa wahisani, kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Mashirika ambayo yatafanya udanganyifu kwa kutokuweka wazi taarifa zao. 


Akizungumza  katika kikao cha jukwaa la Mashirika yasiyo ya kiserikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Kaganda amesema  Wilaya hiyo itafanya Msako  kubaini Mashirika  yanayofanya kazi kinyume na utaratibu na yasioleta  tija kwa jamii hivyo kukwamisha azma  ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo  kwa wakati.


Kaganda ameyataka  mashirika yote yanayofanya  udanganyifu  ikiwa ni pamoja na ubadirifu wa fedha  za miradi  toka kwa  wahisa  kuacha mara moja ambapo ameiagiza Halmashauri kufanya ufuatiliaji  kujua bajeti  na shughuli shughuli zinazofanywa na mashirika hayo.


" shirika linapata mamilioni ya fedha toka kwa wahisani linatekeleza mradi wenye thamani ya  asilimia  1% ya fedha" amehoji Kaganda


Kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Meru  Mwl.Zainabu Makwinya  amesema utambuzi wa Mashirika  yasiyo ya Kiserikali  unaendelea ambapo pia ameshukuru  mashirika ambayo yanashirikiana na Serikali katika swala zima la  maendeleo.



Kwa niaba ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali  Vicent Uhega ambaye ni Mwenyekiti wa Mashirika  yasiyo  ya Kiserikali  halmashauri ya Meru  na Mkurugenzi wa Shirika  Voice of Youth  Tanzania  amesema mashirika hayo yataendelea  kushirikiana na serikali kwa uwazi na ukaribu  ili kuwaletea wananchi maendeleo .


Jukwaa hilo la Mashirika  yasiyo  ya  Kiserikali  limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri  ya Wilaya  ya  Meru  na kujumuisha wawakilishi wa Mashirika  mbalimbali  yasiyo  ya Kiserikali  yaliyopo katika Halmashauri ya Meru .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS