Header Ads Widget

BARABARA YA SAME- KISIWANI- MKOMAZI KM 98 KUJENGWA KWA LAMI



NA WILLIUM PAUL.

UCHUMI wa wananchi wilayani Same mkoani Kilimanjaro hususani Jimbo la Same mashariki ambao ni wakulima wakubwa wa mazao ya biashara unaenda kujua baada ya Serikali kuwaondolea hadha ya ubovu wa barabara ya kufikisha mazao yao sokoni kwa kujenga barabara ya Same- Kisiwani- Mkomazi yenye urefu wa kilomita 98 kwa kiwango cha lami.


Hayo yamebainishwa Bungeni, baada ya Mbunge wa Viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri kudai kuwa katika barabara hiyo yapo maeneo ambayo yaliyengenezwa lami vipande vipande lakini kwa sasa imeshachakaa je Serikali kupitia mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo itabomoa lami hiyo au wataendelea nayo.


" Niipongeze Serikali ya Chama cha Mapinduzi ya awamu ya sita kwa kuiona barabara ya Same-Kisiwani-Mkomazi kwani inachangamoto kubwa na niipongeze Serikali kuingia mkataba wa kuitengeneza kwa kiwango cha lami lakini yapo maeneo yamejengwa kilomita 5, kilomita 3 na kilomita 5 na lami hiyo imechakaa je Serikali inampango wa kuendelea nayo au kuibomoa?" Alihoji Mbunge Zuena.



Akitoa majibu Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alisema kuwa, Madaraja ya Kampimbi yapo kwenye barabara ya Same- Kisiwani-Mkomazi yenye urefu wa kilomita 98.


Alisema kuwa, Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo umepangwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni mwaka huu ambapo ujenzi wake utaanza katika mwaka wa fedha 2023/2024 na utahusisha ujenzi wa barabara na Madaraja.


Alisema awali wakati barabara hiyo ikijengwa vipande vipande ilikuwa ni maelekezo ya wananchi wa maeneo hayo kutokana na maeneo yaliyokuwa korofi pamoja na miji.


Mhandisi Kasekenya alisema kuwa, usanifu uliofanyika maeneo hayo yenye lami imechoka na imechakaa hivyo lami hiyo haiendani na usanifu wa sasa hivyo itafumuliwa na kujengwa upya.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI