Asilimia kubwa ya Watoto wa Kijiji cha Libundu kata ya Kiparamnero wanakosea elimu kutokana na kukosa shule ya msingi na kupelekea wanafunzi wengi kuacha shule wakiwa bado wanaumri mdogo.
Wakitoa malalamiko hayo kwa mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo, Watoto hao walisema kuwa wanaomba kujengewa shule ya msingi iliwaweze kupata elimu katika Kijiji cha Libundu
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alimuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa kuhakikisha wanaandaa mpango wa ujenzi wa shule ya msingi katika Kijiji cha Libundu ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya msingi.
Moyo alisema kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya msingi bure na watanzania wote wanapata elimu ya msingi kwa faida ya Taifa.
Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa aliwataka wananchi kuanza ujenzi wa boma Kisha serikali itamalizia sehemu iliyobaki huku wakitafuta njia sahihi ya kuhakikisha wanapata shule ya msingi katika Kijiji cha Libundu.
0 Comments