Header Ads Widget

UWT MKOA WA NJOMBE WAZINDUA MRADI WA SABUNI

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE 


Jumuiya ya wanawake wa CCM Mkoa wa Njombe UWT Imefanikiwa kuanzisha mradi wa utengenezaji sabuni utakaowawezesha kujiingizia kipato na kutoa ajira kwa vijana.


Katika zoezi la uzinduzi wa mradi huo ripoti iliyosomwa na  katibu wa jumuiya hiyo mkoa Bi.Rehema Mbwana imesema hadi sasa wametumia kiasi cha shilingi milioni 10 kati ya milioni 30 zinazohitajika ili kukamilisha mradi huo.




Aidha mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Njombe Scholastika Kevela amesema kuanza kwa mradi huo ni fursa kubwa katika kuwakomboa wanawake wa UWT.


Akizindua mradi huo mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema mradi huo utasaidia kuondokana na tabia ya Jumuiya za CCM Kuomba omba fedha kwa wadau.



Baadhi ya wanawake wa UWT akiwemo Neema Sigala na Maria Lugome wamekiri kuwa mradi huo umewapa mwanga wa kwenda kubadilika kiuchumi.


Katika hatua za awali mradi huo umeonesha matumaini kwenye jumuiya hiyo kwani tayari wamewapa mafunzo ya utengenezaji wa sabuni hizo baadhi ya wanajumuiya pamoja na vijana wengine.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI