Header Ads Widget

"KUTOREJESHA MIKOPO KWA WAKATI KUMEPELEKEA SERIKALI KUELEKEZA KWENYE TAASISI ZA KIBENKI" MHE FYANDOMO

 



Na  Matukio Daima Media, Mbeya



MBUNGE wa Vitimaalum mkoa wa Mbeya, Mh.Suma Fyandomo amesema Serikali ililazimika kusitisha utoaji wa mikopo asilimia 10 kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu kwa sababu kutokuwepo kwa uaminifu na badala yake kuelekeza kwenye Taasisi za Mabenki.



Fyandomo amesema jana wakati akizindua kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Amenye cha Jijini hapa huku akisisitiza mfumo huo utarejesha  nidhamu ya urejeshaji wa mikopo ingawa changamoto itakuwa kwenye riba.




“Changamoto kubwa katika kupata mikopo kwenye Taasisi za kifedha ni riba kubwa hivyo kama wabunge tumeliona na tunaangalia namna na kusishawishi Serikali kuzungumza na taasisi za mabenki kuweka riba ndogo ya mikopo kwa wajasiriamali ”amesema.



‘’Sisi kama wabunge hili jambo tunalifanyia kazi ili tuweze kuiomba Serikali kuwa ni sawa maamuzi iliyotoa kuwa  vikundi vikakopa kupitia benki tuombe zile fedha za vikundi kuwe na riba ndogo ili wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu  wasikwame kukopa fedha hizo na jambo hilo linaenda kukamilika muda si mrefu’’ amesema Mh. Fyandomo.



Mwenyekiti wa Kikundi hicho  Amenye David  amesema kuwa alipata wazo la kuanzisha kikundi ambacho kilikuwa na watu 16 ambapo walikuwa wakiweka akiba ya shilingi 20 kwa wiki ,baada ya hapo walianza kukopeshana kwa kila mwanachama ili waweze kufanya  ujasiliamali.


Kwa upande wake Mbunge Viti Maalim Zanzibar Mariam Mwinyi  amesema Serikali lina malengo mazuri kuona wana nufaika na mikopo na kikubwa amewataka kuwa na  umoja.



‘’Mzidi kupendana katika kikundi ambacho tumekizindua  tunahitaji kisonge mbele zaidi ya hapa  ili muweze kujiimarisha kiuchumi  katika shughuli zenu’’ _amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI