Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI WAMLILIA DIWANI MACHA....



**********

Na Gift Mongi,MATUKIO Daima App Moshi.

Kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata ya Old Moshi Magharibi Menyasumba Macha kilichotokea may 15 .2023 umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini umeelezea kuhusiana na pigo la msiba huo.

Kwa mujibu wa taarifa kwenda Kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima amesema umoja huo kwa masikitiko makubwa wamepokea taarifa za msiba huo ambao pia ni pigo kwa vijana hao.

"Kwa niaba ya UVCCM Moshi Vijijijini kama mwenyekiti nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha diwani wa Old Moshi Magharibi nipende kutoa pole kwa familia ya marehem ndugu na jamaa wa marehemu viongozi Wa kata, madiwani, CCM, Wafanyakazi Wawakilishi wa Taasisi na Makundi mbalimbali"imeeeleza taarifa hiyo

Pia taarifa hiyo imezidi kufanya kuwa "Kwa heshima na taadhima ninaomba kuwasilisha salaam zetu za rambirambi kwa familia ya Diwani Macha. Ni vigumu kuelezea simanzi iliyoipata Jumuiya ya UVCCM. Taarifa za msiba huu mzito zilitufikia asubuhi ya tarehe 15. Tulichukua muda kumtafakari shujaa wetu diwani wetu tutamkumbuka sana kwa michango yake mingi na mikubwa sana hasa katika jumuiya yetu"imeeeleza taarifa hiyo

Aidha umoja huo unaeleza kuwa marehemu diwani Macha atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kujenga jumuiya kwa ushauri na taaluma yake lukuki pamoja na uongozi wake katika Chama,

"Kwa wale waliobahatika kufanya kazi nae enzi za uongozi wake wanamkumbuka kama kiongozi shupavu na mwenye uweledi wa hali ya juu hakika hii ni hazina haitasahaulika"inaeleza taarifa hiyo

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya mwenyekiti amesema kuwa kwa wengi ambao wamepata nafasi ya kufanya kazi na diwani Macha alikuwa mwanazuoni mwenye maneno machache na sauti ya kiongozi, mwenye msukumo wa kujenga taaluma na Chama mwenye mapenzi ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

"Hata pale alipoonekana amechoka, hakutaka wananchi wake wakose usimamizi thabiti Tuna mengi tumejifunza kwa Diwani Macha na hakika tutaendelea kumuenzi"anaeleza Shirima katika taarifa yake hiyo.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro Ester Maleko ameelezea kusikitishwa na msiba huo

"Nimepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa. Natoa Pole kwa familia na Chama cha Mapinduzi na wananchi wote wa Old Moshi Magharibi hakika Tumempoteza jemedari na kiungo muhimu sana tena mchapakazi alietuwakilisha vyema" anasema Ester

Marehehemu Menyasumba Macha alipata ajali usiku wa may 15 eneo la mjorohoni wilayani Moshi na kusababisha umauti ..

Bwana ametoa, na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Roho ya Marehemu Diwani Macha ipate Rehema kwa Mungu, Ipumzike kwa Amani

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI